Am 27, she is 19.nataka nimwoe,imekaaje??

Hapo juu kwa sithole # 12 si kweli.

Umuoe lakini usikwepe majukumu.

Mimi nilioa at 33 mke wangu akiwa 19 kijijini kabisa 30 yrs ago. Nilimpeleka shule ya ushonaji (ya kiveta veta) mara tu nilipomleta mjini. Ndugu zangu wote 4 ambao walikuwa wamekamilisha masomo yao vyuo vikuu wakati huo, walinitenga kwa kuoa mwanamke asiye na elimu; nikayakubali tu kwani dhamiri yangu iliniambia nafanya kitu sahihi.

Baada ya masomo nikampa mtaji ajitegemee kwa ushonaji, alifanya hivyo. Sasa hivi nimestahafu ananilisha na watoto ambao wanakamilisha masomo yao anawalipia kwa kazi ya ushonaji.

Juu ya sexual life usipime maana ukweli unabaki kuwa gari bovu halikokotwi na gari bovu, thanx to to the age difference; tunafaidi sana na tupo wawili tu nyumbani kwani watoto wana maisha yao na watoto wao. Wajukuu are just friends.

Ndugu zangu wa vigezo vya shule kichwani kati ya 4, mmoja tu amedumu na ndoa, watoto wa ndugu zangu wengine na ndugu zangu wote wanamuangalia huyu mke wangu kama mama yao wakuwashauri.

Tofauti ya umri ina faida moja kubwa unaweza kumfinyanga mwenzio kwa matakwa ya kuendana na maisha yako; mama analea watoto wake full time na kujenga mshimano wa familia (No house girls). Hasara yake ipo 1. atakosa nafasi nzuri ya kusoma, lakini elimu haijawasaidia wengi hasa kwenye kujitegemea. 2. Mwanzoni atajiona yuko out of place kwa udogo wake; baadae anajua na kushika nafasi yake kwenye nyumba kama mama kwa matakwa yenu.

MUHIMU NI WEWE UJUE WAJIBU WAKO UMUELEWE NA UMPE KILA MSAADA ANAOSTAHILI. UWE NA DHAMIRA YA MUDA MREFU YA KUKABIRI CHANGAMOTO AMBAZO LAZIMA ZITAKUWEPO.

Samahani kwa maelezo marefu lakini that is my experience you can share it with me.
 
Gari bovu halikokotwi na gar bovu. Uzee n busara Mimibaba
 


Nani kakwambia kwamba Mwanamke akifika 40's ndiyo damu inachemka sana? Kama katika Umri huo inachemka je huo umri wake wa sasa wa Miaka 18 inatokota? Swala sio saana Umri,swala je wana Afya Njema?(Km issue ni Ngono!) Mwisho kabisa,lililo Kuu ni Upendo!!
 

Haririiìii cherekochereko baba kapata mama,mama kapata baba u wapi ee u wapi mamaake harusi uje hapa tuahangaike nao
 

hahahahahaaaa,,,,,,hiyo risech kaka imenivunjia ukimya nilokua nao hapa ndani,,,,,,,,dah,haya bhana
 
Acha asome akifika angalau 25yrs ndio unaweza kutaka kumuoa...kwa sasa tafuta mwenye umri angalau 23yrs kwenda juu...19yrs atakuja kukusumbua baadae hajui mambo mengi akipata shida kidogo tu atasema sikujua kuwa maisha yana sides 2 tofauti heri niosinge.......najuta!!!
 
Kama hasomi OA
Zubaa mapedeshee waje wakuminyie.

Afu, miezi 6 tu unataka kutangaza ndoa? Mbona anakuharakisha hivyo? Kuna nini behind the scene? au ushamjaza ma voda fasta?

Ila oa tu, mengine mtambua mbele kwa mbele
Kongosho, kuna jamaa nawafahamu wamefahamiana Feb na sasa wameshaoana.................. sina uhakika kama hizi wiki 2 ambazo wapo kwa ndoa they are happily married!
 
Last edited by a moderator:
Kongosho, kuna jamaa nawafahamu wamefahamiana Feb na sasa wameshaoana.................. sina uhakika kama hizi wiki 2 ambazo wapo kwa ndoa they are happily married!

Kuna watu waliwahi kuoana baada ya kufahamiana kwa wiki moja na wapo gado.
 
Last edited by a moderator:
Mpeleke chuo ile kwako!
 
Kama wewe mwanamume ndo ungekuwa 19, ningekueleza usithubutu...ila kwa maelezo uliyotoa, najaribu kutafuta tatizo (la kisheria au kijamii) ila silioni!!

Babu DC!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…