AM FINISHED!!! You ladies why?????

Pole sana mkuu Timbala kwa kuingizwa mkenge.
Sasa hivi kwa akina dada wengine maofisini, hata walioolewa kutembeza "biashara" kwa ajili ya kipato ishakuwa fair game kwao.

Katika mazingira yaliyopo huyo dada kwa vile anaendelea na "biashara" hapo hapo kazini atawakoroga sana ili" biashara" yake ishamiri.
Cha kufanya ni mtonye bosi -halafu utafute kazi nyingine, na kwa hali iliyopo wewe inawezekana hauko peke yako kuingizwa mkenge hapo ofisini.
 

Kama anakuponda kwa jamaa wa kazini kwenu hapo wewe sasa mwaga ugali mwambie mmewe awafumanie
 

Hili linawezekaa sana bi mkubwa,
kwanini uanze kupoteza muda wa kutaka kujua habari zake za ndani,
sijui tabia, sijui mienendo yake, kwani inakuhusu nini.................
wakati unataka ugonge tu na kukimbia....................
mwanaume atahitaji tu kuyajua hayo ya ndani kama tu ana mpango mzima na wewe.....lol..
 

nimeshindwa kuoanisha title na content kabisa... KWELI YOU ARE FINISHED!!
 
Kumbe ndio zako ee, sasa mwenzako kanasa kwa mke wa mtu , atajiju, si unaona roho inavomuuma alivochukuliwa?
 
Hivi nyie vijana wake za watu wa nini na sie wasichana single tumejaa tele
 

Next time usiparamie ovyo vilivyogharamiwa!..mumewe angekufumania ndiyo ungekuwa finished kwelikweli!..
Kukutana kote, kuongea plus mawasiliano ulishindwa kujua ana mtu? labda kama mumewe haishi mji mmoja na nyie..teujenge tabia ya kuchunguzana, mke wa mtu ni sumu!!.
Utulie sasa na huo mshahara wako!
 
Mbona unachoka haraka hivyo? Wanaume mmezoea kuwatenda wanawake siku mkitendwa nyie mnaumia sana. Pole mwaya na hao wapenzi wapya wapotezee tu mwishoni watatafuta topic mpya za kuzungumza
 
Though trusting a partner is a wise attitude, only fools may do.....! So, better you have got a lesson for the future...!
 
Mkuu hongera sana kuweza kujiepusha,mi pia ilinikuta kama hicho ila hajaolewa bali alikuwa anaishi na mtu wake pamoja sema tu hawajafunga ndoa,nilimpenda sana na sikujua kwamba yuko hivo.
Wanawake wa aina hizo wanasababisha watu kwenye majanga ya ajabu hawana lolote,shame on them.
 

1. Mwanamke 'alikupenda ghafla' - Upendo wa kweli hauwezi kuwa wa ghafla..true love takes time to grow and mature
2.Inaonesha ni mwanamke aliyekuwa anaamua uhusiano wenu uendaje - aliyekuwa ameshikilia mpini
3.Hukutaka kumjua kwa undani - ndio maana alikupata kiurahisi
4.Wewe ulikuwa na shida ya ngono tu (ndo maana ulikuw kipofu na kiziwi

Hii inanifundisha kwamba
1. Hukuwa na mawazo au kujipanga vyema kutafuta msichana wa kumuoa - Kwa sababu ungekuwa na mipango hiyo ungekuwa makini kumjua huyo msichana kwa undani - ingekusaidia kujua ni mtu wa namna gani kabla ya kuji-commit kwake
2. Wanandoa ni wasiri kuzungumzia shida za mambo ya mapenzi - inaonesha labda dada alikuwa haridhiki na tendo la ndoa, ilipaswa alizungumze vyema na mumewe; au wamamezungumza lakini hawajafikia muafaka.
3. Huenda alifuata hela zako (kama ulivyojigamba kwamba una mshahara mzuri)


Hivyo basi upenzi wenu ulijengwa katika mazingira ya UZINZI, wewe ulifanya fornication mwenzako adultery.
Tunaambiwa kwamba aziniye na mwanamke hana akili kabisa, na anafanya jambo litakalo angamiza nafsi yake.

"With persuasive words she led him astray; she seduced him with her smooth talk. All at once he followed her...till an arrow pierces his liver, like a bird darting into a snare, little knowing it will cost him his life."
(Proverbs:7:21-22)

Kwa hiyo hata kama asingekuwa ni mke wa mtu, bado ulipaswa kumjua nje ndani..na siku zote UZINZI wa aina yeyote ile una Madhara yake mabaya..Ni kama vile unapotembea kwenye makaa ya moto na miguu peku ni lazima uungue..

Wanaume na hata akina dada, mapenzi ya kweli sio lazima yaambatane na uzinzi ( siku hizi tumepunguza makali tunaita ngono). Get to know somebody inside out before commiting fully. Failure to do will put you into trouble; and you will end up regreting your whole life;

 
Isije kuwa mke wangu!!! ... Unafanya kampuni gani mkuu?
 
Mh. Kwanza nikupe pole. Ila wewe ni wa ajabu kidogo au ni mkimya? Maana mi navyowajua wanaume kweli usijue kuwa mdada ni mke wa mtu na mko same office? hata kama ni mgeni kwa nini ukuuliza wenzako ? Au na wewe ulikuwa na nia ya kupita tu kwa kujifanya mjanja kumbe umepatikana. Maana ungekuwa umempenda kweli huyo dada na ungekuwa na nia nzuri nae lazima ungeuliza kwa wenzio.

Pole ila najua umejifunza. Na naona huyo dada mwenzetu yawezekekana ana maradhi na anatafuta wa kufa nae, haiwezekani abadili wanaume same office. Atawapukutisha shauri yenu. Ukute wewe si wa kwanza hapo ofisini na huyo alo kureplace si wa mwisho. Mtaunga trela sana msipokuwa makini.
 
Dogo hakuna aliyekumaliza, umejimaliza mwenyewe... huweza kuleta excuse kwamba sikujua ameolewa, you can be serious

You cant date a woman without knowing her whereabouts

nasty lie, we sema roho inauma ameamua kuwa na mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…