Ama kweli...Haina Kufeli

Ama kweli...Haina Kufeli

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
"Haina Kufeli"...msemo ambao Mchezaji anayekipiga katika ligi kuu ya Ubelgiji anautumia mara nyingi akimanisha katika maisha usikate tamaa.. kile kipawa ulichopewa na mwenyezi Mungu basi Kwanza mshukuru halafu kifanyie kazi kiwe kikubwa zaidi na zaidi kikuletee pesa kama si mafanikio ...

Sasa Mbwana Samatta anatarajiwa kugombaniwa saini yake na timu hizi...West Ham United, Burnley, Everton, na Brighton .. ina mana mwenye dau zuri la kumsajili na mshahara mnono ndie atapata saini yake...huko katika hizo timu atakutana na akina Chicharito, Yeri Mina, akina Marko Arnautovic, akina Jack wilshere, Theo Walcott na wengineo...

Si ajabu one day tunaangalia super sport 3 HD tunaona Everton labda na Manchester United wamepanga line kabla ya kuingia uwanjani tunamuona kijana wa kitanzania anasalimiana na Romelu Lukaku na Alexis Sanchez.. tayari kuingia pale old Trafford kumenyana ...ama kweli "Haina Kufeli".



501550080-1206x602.jpeg
 
Back
Top Bottom