Ama kweli huduma ya afya ya Zanzibar haitokuwa na tofauti na Uingereza

Ama kweli huduma ya afya ya Zanzibar haitokuwa na tofauti na Uingereza

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Haya mambo mengine bora mtu ucheke tu upate thawabu.

Hakuna Watu waongo katika Dunia hii kama Wanasiasa.



 
Muktadha ni muhimu.

1. Je hii ni kauli ya kisiasa? Kauli za kisiasa zina uongo mwingi, ulaghai mwingi. Kwa kweli wanaoelewa dunia inavyoenda wanajua kwamba kauki za kisiasa zina leseni ya kupindisha mengi kisiasa.

2. "Huduma ya afya ambayo rais Mwinyi ameitamani na ameiweka haitakuwa tofauti na ya Uingereza" maana yake nini?

Huduma hii ni iliyowekwa au iliyotamaniwa?

Kilichowekwa ni kipi na kilichotamaniwa ni kipi?

Mwanasiasa hapo anaweza kujuambia kwamba alikuwa anaongelea huduma iliyotamaniwa kwa nipango iliyowekwa, kwamba kuna aspirations za kuwa na huduma kama za Uingereza. Na akawa sawa.

Hivyo, inabidi tuhoji muktadha na matumizi ya lugha.
 
Kwanini asiseme itakuwa sawa na Tunisia, Libya, Iraq, Irani, Dubai yaani nchi za Middle East? Kweli Dunia ya Mungu, vitu vya mzungu.

Mtaani ukiwa na chuki, hasira muda wote na ugomvi wanakuita mwaarabu ila ukiwa una roho nzuri, watu wakikufanyia kazi unawapata hela yao tena na unawaongeza na ya soda, unafika sehemu kwa wakati, una simu kali, nadhifu, unacheka na kufurahi na kila mtu n.k wanakuita mzungu.
 
Back
Top Bottom