Ama kweli kikulacho kinguoni mwako

Subira the princess

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2018
Posts
3,474
Reaction score
3,744
Wasalaam
Hakika ni vigumu sana kuamini kama huyu mwamba mbowe anashirikiana na ccm watesi wa wanachadema. Kuna watu wamepoteza maisha kukipigania chama, na kuna watu ni vilema, mpaka leo Tundu lisu anatembea na risasi mwilini kwa sababu ya chadema.

Swali la kujiuliza ina maana muda wote huo mbowe anawala wenzie kisogo huku akishirikiana na watesi? Je kuna namna alihusika kushirikiana na ccm kuwapoteza na kuwaangamiza baadhi ya makada chadema? Yaani nawaza tu kwa sauti kubwa.

R.I.P Mzee wetu Ally Kibao mola akuepushe na adhabu ya kaburi.
 
Watanzania yafaa tuwaze na kuwazua,na tujitafakari kweli kweli.
 
Naomba nipingane na wewe kuhusu risasi za Lissu! Hizo hazijatokana na kukipambania chama bwana! Hizo ni shauri ya ubishi wake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…