Ama tukubali Kufa au Kupona!!

Ama tukubali Kufa au Kupona!!

Kigarama

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2007
Posts
2,492
Reaction score
1,230
Kwa kufeli huku kwa wanafunzi wa Kidato cha nne (wote siyo watoto) ni lazima tufanye uamuzi ama wa Kutumia Kiingereza au Kiswahili Kufundishia Maarifa kwenye taasisi zetu za Elimu. Kama maarifa hupitishiwa kwenye Lugha basi Lugha ni chombo muhimu sana kwenye kujenga Elimu Imara kwenye jamii yoyote ile.

Kama tunaamini Kiswahili hakifai kufundishia ni lazima tukiondoe kufundishia kuanzia darasa la Kwanza hadi la Saba badala yake tukikumbatie Kiingereza,na kama tunadhani Kiingereza kimeshindwa kututoa hapa tulipo, basi tuachane nacho na kurudi kwenye kutumia Kiswahili katika kufundishia Maarifa kwenye taasisi zetu za Elimu hapa nchini!! Uamuzi huu ni LAZIMA ufanyike sasa.
 
Kwa kufeli huku kwa wanafunzi wa Kidato cha nne (wote siyo watoto) ni lazima tufanye uamuzi ama wa Kutumia Kiingereza au Kiswahili Kufundishia Maarifa kwenye taasisi zetu za Elimu. Kama maarifa hupitishiwa kwenye Lugha basi Lugha ni chombo muhimu sana kwenye kujenga Elimu Imara kwenye jamii yoyote ile.

Kama tunaamini Kiswahili hakifai kufundishia ni lazima tukiondoe kufundishia kuanzia darasa la Kwanza hadi la Saba badala yake tukikumbatie Kiingereza,na kama tunadhani Kiingereza kimeshindwa kututoa hapa tulipo, basi tuachane nacho na kurudi kwenye kutumia Kiswahili katika kufundishia Maarifa kwenye taasisi zetu za Elimu hapa nchini!! Uamuzi huu ni LAZIMA ufanyike sasa.

Kigarama tatizo siyo lugha maana hii mitaala ndiyo tuliyofundishiwa zamani lakini hatukufeli kama hawa...........fikiria kwenye chumba cha mtihani mtu anaandika matusi jiulize ana malezi gani na anaionaje elimu hii katika maisha yake?

Elimu hii haina uhusiano mkubwa na maisha yao na ndiyo maana hawaithamini.........tujiulize hii elimu mbona hata sisi tuliyoipata hajilisaidia taifa na hawa wanaliona hilo na ndiyo maana wanazama katika maisha mafupi ya ngono tupu............
 
Mkuu Kigarama,sidhani kama tatizo letu kubwa ni lugha.
Mbona Kiswahili kinaeleweka kwa watanzania wengi,lakini bado hali ni mbaya kwenye shule zetu za msingi?
Nadhani kuna tatizo kubwa kwenye:

1/MITAALA YA KUFUNDISHIA.
Mitaala yetu ya kufundishia si relevant na mazingira halisi ya watanzania tunayo ishi.
Mwanafunzi anasoma maeneo ya vijijini ambayo kazi kuu ni kilimo na ufugaji;badala ya mwanafunzi kuwa trained ku acquire skills za kuweza kuendeleza maeneo haya,mwanafunzi anafundishwa vitu irrelevant kabisa.
Hii hupelekea mwanafunzi kupoteza mori wa kujisomea na kupelekea kufeli.

2/MASLAHI DUNI YA WALIMU.
Hii imepelekea kuwa na mgomo baridi wa walimu,baada ya kuona wanapuuzwa na serikali yao.
Kwa mazingira haya kufeli ni inevitable.

3/ALAMA ZA KUFAULU ILI KUJIUNGA NA UALIMU.
Inasikitisha sana kuwa ualimu umegeuka kuwa taaluma ya wale "walio feli"!
Kwa mfano,wale walio maliza form four na kupata div. 1V,hivyo kushindwa kuendelea A Level,huenda ualimu wa shule za msingi.
Mambo ni yale yale kwa diploma na hata degree za ualimu.
Hii inachangiwa na MASLAHI DUNI ya walimu,hivyo mtu akipata marks za juu,kamwe hatapenda kwenda ualimu(with few exceptions).
Sasa tutegemee nini toka kwa hawa walimu "walio feli"?

Sasa ndugu Kigarama,ili tutoke hapa tulipo,ni vyema kuyaangalia haya yote kiundani,badala ya kudhani Lugha ndio tatizo pekee.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Kigarama,

Mimi nalitazama suala hili kama tatizo la qualitative INPUT katika mfumo mzima wa elimu e.g. ukosefu wa walimu bora na badala yake serikali inawekeza katika bora walimu, serikali haiji with enough allocation of resources kupitia bajeti kila mwaka, kukosekana kwa a proper regulatory authority kwa ajili ya sekta ya elimu ngazi ya msingi na sekondari ili kusimamia vyema suala la mitaala, ukosefu wa motivation ya walimu kutumikia sekta ya elimu - kwa mfano walimu wapo kwenye mgomo baridi kwa miaka mingi sana kutokana na profession yao kupuuzwa kwa kila hali; ukosefu wa motivation ya wanafunzi kufanya vizuri - kwani wananafunzi wengi wanakosa motisha kutokana na kukosa uhakika wa educational outcome wakimaliza shule huku pia wakiwa na uelewa fika kwamba taifa linafuata mfumo wa elimu zaidi ya mmoja na kila mfumo unaendana na hali ya mfuko wa familia husika (nguvu ya soko, sio serikali tena), pia kutokana na udhaifu wa serikali katika kuwapatia watoto wa taifa motivation, inspiration, kushindwa kuwalinda katika na kuwatetea kikamilifu kuhusiana na suala la access to quality eduaction n.k; Haya yote ni sehemu ndogo tu ya INPUT ambayo Serikali imeshindwa kuisimamia ipasavyo, na matokeo yake, lazima OUTPUT itakuwa ni ya Ovyo ovyo tu;

Suala la Lugha sidhani kama linachangia kwa kiasi kikubwa kwani kwa mfano wapo wachina, wahindi, wa-srilanka n.k, ambao ikitokea wanapata nafasi kwenda nje kusoma vyuo mbalimbali kwa lugha ngeni kabisa - kiingereza, kwa vile serikali zao zimewaandaa ipasavyo in terms of INPUT, kinachofanya wafanikiwa huko nje ni motivation yao ya kujifunza bila kuchoka kwani wanajua jinsi gani serikali zao zinavyo thamini elimu kwa vitendo na vile vile in one way or anotherw, wanajua kwamba the education outcomes (wanasoma ili iweje) on their part itakuwa ni positive at some point, sio suala la bahati nasibu;

Tukiwekeza katika input, hakika process itakuwa na tija na kutupatia output nzuri; Mwisho tujiulize, je inakuwaje mataifa yenye mafanikio makubwa kuliko yote duniani kiuchumi kama Uingereza, Canada na Marekani ambao English ni lugha yao kubwa, kwanini katika rankings za ubora wa elimu among countries wote hawa hawapo katika tano bora bali mataifa mengine ambayo english ni second if not a third language? Ebu tazama orodha ifuatayo ya top 20 educational systems in the world (source bbc.com):


  1. Finland
  2. South Korea
  3. Hong Kong
  4. Japan
  5. Singapore
  6. UK
  7. Netherlands
  8. New Zealand
  9. Switzerland
  10. Canada
  11. Ireland
  12. Denmark
  13. Australia
  14. Poland
  15. Germany
  16. Belgium
  17. USA
  18. Hungary
  19. Slovakia
  20. Russia
 
Back
Top Bottom