Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Taarifa kamili hii hapa
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA-Bara Mhe Amani Golugwa leo amefika ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kufuatia wito wa Polisi uliotolewa kwake na Jeshi hilo tarehe 24 Februari 2025.
Mhe Golugwa alisindikizwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Bara Mhe John Heche, Mjumbe wa Kamati Kuu Mhe Godbless Lema na Wakili wa Kujitegemea Hekima Mwasipu
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Baada ya kufika ofisini Kamanda wa Upelelezi wa Mkoa Davis Msangi - SSP alimweleza Mhe Golugwa atoe ufafanuzi wa kitu gani kimepangwa kufanyika tarehe 27/02/2025 kupitia kauli ambayo amesikika kwenye video fupi jongefu akizungumza katika kuhamasisha kuhusiana na tukio la kichama linalokusidiwa kufanyika tarehe hiyo.