Amani Golugwa: Kama chama tuna mashaka na kifo cha Maradufu

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Naibu Katibu Mkuu Bara - CHADEMA, Amani Golugwa amesema kuwa chama kinatilia mashaka kuhusu kifo cha aliyekuwa dereva wa John Heche

Your browser is not able to display this video.

Mama mjane na wana Tarime naomba niwaambie jambo moja. Na mnisikilize kwa makini mtuelewe. Sisi kama chama, tuna mashaka na kifo cha Suezi Maradufu.

Tumefanya uchunguzi wa hatua ya awali kwa mambo yanayoonekana kwa macho. Mabingwa... hatua ya awali, kilichopelekea kifo chake ni mshipa unaopeleka damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye kichwa, ule mshipa damu iliganda kwa kiwango kikubwa sana. Na hivyo ikapelekea shinikizo lile kuwa la nguvu na... fursa yoyote ya kuishi.

Lakini sasa, jambo gani limesababisha hilo shinikizo la ghafla damu kuganda, ndilo jambo la kiuchunguzi ambalo sisi tumesema tunataka tupate taarifa ya kisayansi. Hivyo tunawaomba familia na wana Tarime, mtuunge mkono mkubaliane na sisi kwamba tunataka tupate u... Katika uchunguzi, zilikuwa zimegeuka na kuwa za bluu. Mtaalamu akatuambia... ndani au nje linaloweza kusababisha kwamba alitendewa jambo fulani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…