Amani na utulivu wetu uliishia mwaka 1995 hapa tanzania

Amani na utulivu wetu uliishia mwaka 1995 hapa tanzania

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,356
Reaction score
16,379
Wengi mtakubaliana na mimi kwamba amani na utulivu wetu kama nchi mwisho wake ulikuwa 1995
Baada ya hapo amani na utulivu wetu tuliviweka rehani pale tulipoanza kubinafsisha kila kilicho chetu kwa watu binafsi kutoka katika umiliki wa serikali bila umakini

Na kwa watu wenye mapenzi mema na nchi au wazalendo wa nchi hawawezi kukaa kimya kuona mali zetu wamepewa watu bila sisi kujua tunanufaika vipi
Hapa ndipo walioiweka rehani amani na utulivu wetu walipoyaangalia matumbo yao tu huku nchi ikibski yatima bila mtetezi kwa kuwa alibinafsisha mali ya nchi bila umakini hakuwa na uwezo wa kuongea wala kukemea na hapa ndipo tuliwahitaji watu majasiri wa kusema tunapoelekea sipo na watu hawa hawakuwa ndani ya serikali bali nje ya serikali

Na hapa ndipo tulipojua umuhimu wa vyama vya upinzani
Hapa ndipo tukajua nini umuhimu wa kuwa na vyama vya upinzani
Msjasiri kutoka ndani ya vyama vya upinzani walianza kuonyesha namna serikali ilivyobinafsisha mali ya watanzania bila kuangalia maslahi yao wao

Na hapa ndipo amani ya nchi na utulivu wake ulipopotea na sasa naweza kusema amani na utulivu kwa Tanzania haupo tena kwa kuwa waliosababisha yote haya hawataki kuambiwa ukweli na sasa hujiona kama malaika
Huku wakiapa kuua kujeruhi kwa watakaonyesha kimbelembele katika hili
 
unaweza kuwa sahihi.lakini la muhimu ni je tuko tayari kufanya chguzi za haki?.pia amani kuwepo inahusisha mengi.ikiwemo mishahara bora,mazingira bora ya wanafunzi na miundombinu rafiki mijini na vijijini.kama hivyo nilivyotaja vinapatikana kwa kubip basi unaweza kuwa kweli.
 
Ujio wa Mkapa ndilo jambo la hatari zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya nchi hii.
Hatari kuliko hata Ujio wa Mkoloni au Uvamizi wa nduli Iddi Amin Dada kule Kagera.
Kaondoka miaka 13 iliyopita lakini hadi vizazi vya mwaka 2090 vitalipia madhambi yake!
 
Ujio wa Mkapa ndilo jambo la hatari zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya nchi hii.
Hatari kuliko hata Ujio wa Mkoloni au Uvamizi wa nduli Iddi Amin Dada kule Kagera.
Kaondoka miaka 13 iliyopita lakini hadi vizazi vya mwaka 2090 vitalipia madhambi yake!
Siyo kulipia dhambi...bali ni kuonja madhara ya dhambi za mkapa...
 
Back
Top Bottom