Makuri Paul Chacha
Member
- Oct 21, 2010
- 39
- 34
Leo ni siku muhimu sana kwetu Tanzania. Tunapata fursa nyengine muhimu ya kukubaliana na watawala, tunahitaji nini kwa miaka mitano ijayo.
Uchaguzi ni vita ya maneno, sera, hoja na mikakati ya kutafuta ushindi kwa mtu mmoja na kwa vyama pia. Kwa takribani miezi 3 mapambano hayakuwa mepesi toka ndani ya vyama hadi uchaguzi wenyewe.
Siku ya leo Watanzania kwa wingi wetu tumejitokeza kutimiza wajibu wetu na haki zetu. Imebaki sehemu muhimu. Kuhitimisha. Yaani kuhesabu kura, kutangaza matokeo na kupokea matokeo.
Hatua hii ni muhimu sana. Natoa wito wahusika wote kutimiza wajibu wake, kwa kulenga amani na mshikamano wa nchi yetu.
Haki itendeke, upendo utawale, masilahi ya wengi yazingatiwe, wagombea na wafuasi wao waridhike na uamuzi wa wananchi walio wengi.
Amani yetu, maendeleo yetu, Taifa letu. Tanzania kwanza.