Ambangile wa WASAFI FM atoa maoni take kuhusu usajili wa Haaland United

Ambangile wa WASAFI FM atoa maoni take kuhusu usajili wa Haaland United

Matanga

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2019
Posts
2,281
Reaction score
3,976
*Maoni ya mchambuzi george ambangile [emoji1541]*

Haaland au Greenwood .

Naona Manchester United wanahusishwa na Erling Haaland ambaye ana miaka 19 wakati tayari kwenye kikosi chao wana Mason Greenwood ambaye ana miaka 18 na uwezo mzuri wa kuweka kambani .

Hoja yangu kubwa ni hivi, ni kweli Man United wana uhitaji wa straika lakini straika huyo binafsi naamini anatakiwa kuwa yule wa daraja la Dunia ambaye tayari ametimia mithili ya Robert Lewandowski, Harry Kane na wengineo ambao kijana kama Greenwood atajifunza kutoka kwao .

Lakini ukisajili kama Haaland mwenye miaka 19 itakuwa inatuma ujumbe gani kwa Greenwood ? Ndio Halaand ni mmazaliziaji mzuri sana lakini pia amepata faida ya kucheza klabu ambayo anapata sana nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza , vipi Greenwood akienda klabu kama Salzburg na kuanza kuweka kambani mara kwa mara kwasababu ya kupata nafasi ya kucheza kama Haaland ....baada ya hapo atanunuliwa kwa kiasi gani ? .

Nafikiri United wana sehemu nyingine za kipaumbele zaidi za kuimarisha kabla ya Haaland hasa ukizingatia haijulikani mustakabali wa Paul Pogba .

Option iliyobaki labda kama Man United wamsajili Haaland halafu mmoja wao baina ya Halaand na Greenwood kutolewa kwa mkopo , kama ikitokea Greenwood kukubali maana wengine huwa wanakataa mkopo na kutaka kuuzwa moja kwa moja . Kwasababu kama unataka kumpa nafasi Halaand kwanini usimpe Greenwood ? Ili mashairi yako yaeleweke vizuri kwa Mason basi ingia sokoni na kusajili straika wa daraja la Dunia ambaye ameshawahi kujaribiwa katika ngazi ya juu na kutoa mazao sahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sina mengi, lakini mchezaji wa kariba ya Haaland hastahili kutua Manchester united ila Borussia Dortmund na Chelsea, Haaland ana uwezo mkubwa wa kufumania ny'avu ila kwa Manchester United hatapata game time ya kutosha japo wenyewe wanasema ni Dreaming theatre!
.
Mason Greenwood ni bonge moja la striker ila hapati game time ya kutosha akicheza sana ni 15 minutes, endapo Haaland akitua United basi Greenwood atahitajika kucheza pungufu ya dk 10 na mechi chache zaidi, ni mtazamo wangu
 
Halaand akiongezeka katika kikosi cha utd,atafiti kutegemea na mifumo ya kocha itakayoendana naye,uwepo wake utasababisha ushindani kati yake na greenwood hivyo kufanya timu kuimarika katika eneo LA ushambuliaji na kuweza kuiletea matokeo chanya,ukiangalia kwa sasa mfumo Wa kutumia vijana imekuwa ukisaidia kuleta matokeo mazuri kwa timu kadhaa barani ulaya,ukiangalia timu kama Ajax amsterdam,Bayern munchen,man utd,Chelsea wanafanya vema kabisa,kutua kwake UTD kutaongeza chachu ya mapambano ya mafanikio kwa vijana wanaochipukia kufikia malengo yao.
Atue tu UTD alete changamoto mpya katika kikosi cha vijana Wa OGS.
 
Kuna kipindi Pogba akiwa kinda alikuwa hapo Man United, akaenda alikoenda! Baada ya miaka kadhaa wakamnunua kwa hela ndefu! Naona hili likijirudia kwa kinda fulani pale OT!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekusoma vema mkuu

Back
Top Bottom