Matanga
JF-Expert Member
- Nov 13, 2019
- 2,281
- 3,976
*Maoni ya mchambuzi george ambangile [emoji1541]*
Haaland au Greenwood .
Naona Manchester United wanahusishwa na Erling Haaland ambaye ana miaka 19 wakati tayari kwenye kikosi chao wana Mason Greenwood ambaye ana miaka 18 na uwezo mzuri wa kuweka kambani .
Hoja yangu kubwa ni hivi, ni kweli Man United wana uhitaji wa straika lakini straika huyo binafsi naamini anatakiwa kuwa yule wa daraja la Dunia ambaye tayari ametimia mithili ya Robert Lewandowski, Harry Kane na wengineo ambao kijana kama Greenwood atajifunza kutoka kwao .
Lakini ukisajili kama Haaland mwenye miaka 19 itakuwa inatuma ujumbe gani kwa Greenwood ? Ndio Halaand ni mmazaliziaji mzuri sana lakini pia amepata faida ya kucheza klabu ambayo anapata sana nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza , vipi Greenwood akienda klabu kama Salzburg na kuanza kuweka kambani mara kwa mara kwasababu ya kupata nafasi ya kucheza kama Haaland ....baada ya hapo atanunuliwa kwa kiasi gani ? .
Nafikiri United wana sehemu nyingine za kipaumbele zaidi za kuimarisha kabla ya Haaland hasa ukizingatia haijulikani mustakabali wa Paul Pogba .
Option iliyobaki labda kama Man United wamsajili Haaland halafu mmoja wao baina ya Halaand na Greenwood kutolewa kwa mkopo , kama ikitokea Greenwood kukubali maana wengine huwa wanakataa mkopo na kutaka kuuzwa moja kwa moja . Kwasababu kama unataka kumpa nafasi Halaand kwanini usimpe Greenwood ? Ili mashairi yako yaeleweke vizuri kwa Mason basi ingia sokoni na kusajili straika wa daraja la Dunia ambaye ameshawahi kujaribiwa katika ngazi ya juu na kutoa mazao sahihi.
Sent using Jamii Forums mobile app