Ambao hatukujaliwa mpaka sasa

papag

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
1,156
Reaction score
1,667
Wakuu habari za mihangaiko?

Katika maisha yako ambayo Mungu amekupa mpaka sasa Kuna mipango na mtarajio mengi sana uliyategemea kuyatekeleza kabla ya kufika umri fulani. Lakini mipango si matumizi.

Je wewe yote uliyo panga umeyatimiza? Mimi bado sana sana kutimiza ya kwangu. Karibuni kwa ushuhuda na ushauri..
stay safe CORONA iphoo mleu..
 
mkuu mimi naona ndo naanza alifu kwa ujiti sina hata mpango mmoja ulio tiki zaid ya kununua mashuka getto mambo hayaendi kabisa yan kudadeki
Si bora wewe una getto na unajitegemea bro, mi bado nipo home 24yrs now, ndo najichanga changa nichonge ka kitanda na godoro nisepe japo ni last born nianze kujipambania kivyangu.

Haya mambo ya kula kulala naona kama jau tu, hakuna kitu kizuri kama kukaa na kula chakula ulichokitolea jasho mwenyewe, siyo ugali wa shikamoo unakula huku ukijihisi nafsi kukusuta.
 
Kitendo cha kuwa hai na afya tele tayari ni utajiri namba moja kwa upande wangu.hilo ni lengo namba 1
 
Inaonekana humu JF wengi wao wamefanikiwa malengo yao. Hongereni sana Wakuu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Nakumbuka nilipanga mengi Hadi sasa sijatimiza hata 1

Enzi hizo napanga nikifika miaka 23 nitazaa mtoto now nipo 27 hata dalili Sina

Nilipanga nijiajiri tangu miaka hiyo Hadi Leo naajiliwa

Mengi sijatimiza Mungu anipe ujasiri kwakweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…