Ameacha ufundi electronics yeye anaenda kusomea udereva daraja c

Desierto

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
901
Reaction score
3,112
Hatumzuii au hatumpingi mtu ila tunampa tu ushauri yeye ataamua aubebe au autupe

Kuna mdogo wangu alitoka kijijini juzi kamaliza form4 mwaka jana.

Sasa alikuja kama na laki 3.5 hivi lrngo akasomee udereva. Ila kwa upendo tu nikaona nimpe ushauri wa kuchagua.

Nikamshauri kuhusu ufundi wa simu na redio tv. nk.

Sijamlazimisha ila akapenda. Badi tukaingia mjini tukanunua vifaa vya kazi lengo mm ntakuwa mwalimu wake. Nimekaa nae ofisini muda wa miezi 3 hivi akawa tayari ameshajua baadhi ya kazi kama kubadilisha vioo vya simu mic kubadilisha baadhai ya components kama sisytemy chaja nk. Pia kutambua baadhi ya matatizo ya redio na tv.

Yaani kiujumla yale matatizo sugu ya simu akawa ameshayajua

Pasi hita za maji kutumia mita pia nk.

Sasa kumbe wanawasiliana na mzee kijijini kisiri kuhusu mpango aende veta akasome udereva. Akaenda akatafuta chuo pamoja na kaka mkubwa. Basi wakalipia kozi ya mwezi mmoja 250

Bila kujali mimi nikampa tena ushauri kama ameamua kudili na fani ya udereva basi akomae kweli kweli yeye anataka kuendesha magari makubwa.

Nikamwambia ili iwe rahisi itabidi pia aende gereji ili ajue mambo mengi zaidi kuhusu magari.

Ukweli sisi home ni maisha ya kuunga unga tu

Lengo langu ilikuwa ni akishajua vizuri ufundi afungue na biashara hapo hapo ya vifaa vya electronic.

Sasa naona amenipuuza

Hapa ofisini kwangu nafanya kazi nyingi hivoo nilimshauri akikaa mwaka tu anakuwa amepata mwanga kutengeneza vitu vingi.

Kama vile simu radio tv pasi brenda software kwenye simu ndogo ndogo umeme wa majumbani. Kuunda amplifaya ndogo ndogo. Pia hata biashara na machimbo yake.

Ofisi yangu bado ni ndogo ila kila muda najitahidi kuongeza kipato na mzunguko wa pesa. Sijaandika mahali ila wastani kwasasa kwa mwezi naingiza zaidi ya laki 5 kama faida tu. Kutokea kupata laki 1 miaka mitatu iliyopita.
 

Attachments

  • IMG20261003193703.jpg
    499.1 KB · Views: 15
  • IMG20261003200124.jpg
    505.9 KB · Views: 13
  • FB_IMG_17910470102314366.jpg
    124.8 KB · Views: 14
Muache afanye kile apendacho mkuu hauwezi jua pengine mafanikio yake yapo huko kwenye udereva.
Hata huo udereva hawezi kupata daraja C moja kwa moja kama ndiyo ananza tu
 
Mwenzio passion yake sio technician, ila Driver 🚛.
Muache afanye kile moyo unataka.
 
well done,
umempa ujuzi na maisha, kayataa mwenyewe kwa hiyari yake, wacha akacheki fursa apendayo..

Mruhusu tu,
acha ausikilize moyo wake, atarudi kwa namna nyingine.

umetekeleza wajibu wako kwa moyo wako wote, hakuna wa kukudai wala kukulaumu, songa mbele gentleman 🐒
 
Haya mambo ungemwambia mzee wako akajua na kuelewa isingekuwa shida sasa huu uzi huku ni kma lawama tu kwa dogo na mzee

Lkn pia fani moja 😂 ndugu siyo njema kaka mwache apate leseni mbele kwa mbele ataona yeye kinachomwingizia fedha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…