Jamani kweli hii ni njia panda kwangu, nilimfuma boyfriend wangu akiwa na mrembo mwingine, kwa upendo wangu nilimfata na mkuulza je hapa ndiyo safari uliyoniaga ya kuwa utakuwa mkoani for some weeks?basi badala ya kuanza kunielezea kwanini amenidanganya kuwa yupo safari angali namuona na binti mwingine kwa bar!alianza kunipiga na kuniona kama mimi ni mgomvi kwa kumuuliza kwanini unanidanganya na kuwa na wanawake wengine? Je hii ni sahihi kwa alichokifanya kwangu? Naombeni ushauri wenu nami nitaufanyia kazi
Chanzo: Ladies Chat Blogspot
Jamani kweli hii ni njia panda kwangu, nilimfuma boyfriend wangu akiwa na mrembo mwingine, kwa upendo wangu nilimfuata na kumuuliza je hapa ndiyo safari uliyoniaga ya kuwa utakuwa mkoani for some weeks? Basi badala ya kuanza kunielezea kwanini amenidanganya kuwa yupo safari angali namuona na binti mwingine kwa bar!alianza kunipiga na kuniona kama mimi ni mgomvi kwa kumuuliza kwanini unanidanganya na kuwa na wanawake wengine? Je hii ni sahihi kwa alichokifanya kwangu? Naombeni ushauri wenu nami nitaufanyia kazi
Dada yangu waswahili husema msema pweke hushinda maana hapa umeongea peke yako ingekuwa vizuri kama na huyo mtuhumiwa naye tungemsikia, hapa inakuwa ni vigumu kwa mtu kutoa ushauri kwa kuwa mtu mwenyewe ulimkuta bar inawezekana labda na yeye alikuwa ndio anasubiria muda ufike au labda huyo aliyekuwa naye ni mfanyabiashara mwenzake na wewe inawezekana ulimfikia bila heshima wakati yeye wala hakuwa na nia mbaya ndio yote hayo yakatokea.Ni bora mkatafuta mtu aliye na umri mkubwa zaidi yenu na kila mtu kati yenu aeleze ukweli wa tukio lenyewe na uamuzi ufikiwe.Ni bora kutazama pande zote kabla ya kulaumu na kushutumu.Siku zote ukweli humuweka binadamu huru na ukisema ukweli usikimbie bali simama na utetee kile kilicho cha kweli.
Achana naye njoo kwangu pm please!:A S 8:
we nawe unauliza nin sasa?
hakupend uyo wewe sepa au unampenda sana?
achana nae ebu sepa
uache kumchunguza mkeo, kaa nyumbali, ulikuwa unatafuta nini huko, ndo hasara za kuchunguza chunguza badala ya ktulia, utajuta sasa umeona na umepata stahili yako..