America in equivalence to africa

Idrisa1510

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2018
Posts
254
Reaction score
351
Katika mifumo yangu ya maisha nilijikuta tu napenda mambo ya wamerekani weusi, nlikuwa napenda uvaaji wao "CASUAL" napenda namna wanavyochukulia maisha poa poa, kiasi kwamba nikajikuta na mm navaa zaidi kiamerica, nachukulia vitu poa tu mpaka nione hali imebadilika.

Kuna kipindi ilinigharimu kidogo kwa sababu watu wengi huwa tunaangalia sana mavazi na muonekano, haswa unapokutana na watu flani wanaoamini wao ni waungwana. . . .

Nliwahi kujikuta katika harakati za kumtia "SOUND" dada mmoja mhafidhina wa muonekano, nkaishia kupata reaction flani ya dharau ya kistaarabu. Mtoto akanipandisha, alafu akanishusha, afu akageuka huku anaangalia "American boot" nlokuwa nimevaa mguuni.

Katika kupenda umarekani nikajikuta nfuatilia sana mambo ya marekani huku nikilinganisha na huku kwetu,
Well,

Zamani flani nliwahi kujiuliza kwanini wasanii wa kimarekani walikuwa wanauza copy za CD zaidi ya milioni moja (platinum) kirahisi huku sisi kwetu Tanzania msanii pekee aliyewahi kufikisha platinum moja ni "Mr. Nice" pekee?

Nkagundua mtaji mkubwa walionao ni idadi ya watu ambayo ni karibu mara saba yetu watanzania. Kwa tofauti hiyo ya idadi ya watu, mkilenga percent flani saw ya market, basi Idadi ya wateja wa marekani lazima iizidi ya watanzania (hesabu rahisi tu hizi).

Kwa hiyo kuanzisha biashara kwa business models za America lazima upigwe za uso huku kwetu Tanzania, simply kwa sababu idadi ya wateja wa ndani wao wapo wengi kuliko sisi.

Hii ilinipa kunifikirisha sana haswa pale ambapo nimeamua kujikita katika uwanja wa uandishi wa vitabu, kitu ambacho siyo tu ni nadra kwa watanzania, lakini hata wale niwaowaandikia (wanafunzi wa sayansi wa sekondari) wapo wachache pia.

ANYWAYS,
Siku moja nlikuwa nawasikiliza Strive Masiyiwa na Aliko Dangote wakiwa kwenye conference moja huko Malaysia, wakawa wanazungumzia matatizo yanayofanana katika nchi nyingi za kiafrika, vitu kama urasimu, sera mbovu za kimaendeleo, rushwa, nk, nkagundua kuwa matatizo ya waafrika yanafanana, waafrika wanafanana mila na desturi nyingi, mifumo ya maisha na changamoto zingine, ghafla nkagundua kuwa kuwa nikitengeneza solution ya tatizo flani la Tanzania, kuna uwezekano nikawa nimesolve matatizo ya nchi nyingi tu kwa wakati mmoja, nikajifunza kuitizama Africa kama nchi moja, kama United States of America tu, na hiki ndicho chanzo cha post hii, kwamba ukiitizama Africa kama nchi moja utakuwa na mtaji wa watu 1.2 billion, idadi ambayo inakaribia mara nne ya America, huku majimbo ya marekani ni kama nchi mbali mbali za Africa tu.

Hapa naweza andika mpaka asubuhi, ila lengo langu ni kuwatia moyo young entrepreneurs that we can make real fortune if we look at Africa as one country, think of a solution that can be universal and then go from there.

It is not okay to settle for less and wait for Europeans to tell us that Africa is like a single country when they come and recolonise us again. . . .

Mm nimeshaanza kufanya mchakato wa kuifanya "INSPIRATION SCIENCE PLATFORM' an African module that fits into any country's education system.. . .
Wewe je?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakikisha unahonga sana, unakopa sana na mwisho ujipendekeze sana kwa kila mwanasiasa, hapo ndo utapata usalama katika mradi wowote utakao uanzisha na kuusimamia Afrika.
 
Hakikisha unahonga sana, unakopa sana na mwisho ujipendekeze sana kwa kila mwanasiasa, hapo ndo utapata usalama katika mradi wowote utakao uanzisha na kuusimamia Afrika.

Umekariri ujinga
 
mawazo yako Mazuri Ila afrika bado tuna changamoto nyingi hasa hasa suala zima la miundombinu.

kwa mfano km una bidhaa yako unataka kumuuzia mtu yuko Nigeria , changamoto ya kwanza kbsa ni usafiri, njia pekee iliyopo ni kutumia ndege which is very expensive na changamoto ya pili ni njia za malipo kwa sasa njia zilizopo ni mabeberu na zina gharama sana.

all in all tusubirie sasai app ya masiwyiwa inaweza kuwa mkombozi mkubwa ukichanganyanya na free trade area agreement nadhani mambo mengi yatafunguka.

k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…