Amerika Kusini ni bara hatari mno kwa watetezi wa mazingira kuishi

Amerika Kusini ni bara hatari mno kwa watetezi wa mazingira kuishi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Shirika la kutetea mazingira la Global Witness limesema rekodi ya watu 227 waliuwawa kote duniani mwaka jana wa 2020 kutokana na utetezi wa mazingira. Shirika hilo linasema idadi hiyo ni sawa na watu 4 kila wiki na karibu robo tatu ya vifo hivyo vimetokea Amerika Kusini.

Katika ripoti yake ya kila mwaka, shirika la Global Witness limesema kwa mwaka wa pili mfululizo, Colombia ndiyo nchi ambayo imeshuhudia idadi kubwa ya mauaji ambapo watu 65 waliuwawa.

Ripoti hiyo inazidi kusema kwamba 7 kati ya nchi 10 hatari zaidi kwa watetezi wa mazingira kuishi ziko Amerika Kusini ambapo watu 165 waliuwawa ingawa shirika hilo linasema idadi hiyo ni ndogo kuliko hali halisi ilivyo.

Nchi zengine hatari ni Ufilipino, Brazil, Honduras, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Guatemala, Nicaragua, Perus na India.
 
Back
Top Bottom