Nyamuleha jr
Senior Member
- Feb 20, 2013
- 185
- 65
Kuna mdogo wangu mmoja anasoma secondary form four. Huyo dogo alikuwa mpole tu sana alivyokuwa kidato cha pili na anauwezo mzuri sana darasani, ila alipofika form 3 alibadilika, ghafla akawa haendi shule mara kwa mara, akaanza kuwa anarudi nyumbani, saa sita au saba usiku. Baada ya kufatiliwa alikutwa kumbe. Anavyo acha kwenda shule anaenda kijiweni, na kucheza puli tebo, anafanya vibarua. Baadaye tukawa tunamuonya akawa haskii, mzee alianza kumpiga sana lakini ndiyo alizidisha kabisa, ilifikia kipindi mpaka tulimwita mgambo akimpiga sana ila alikaa siku tatu baadaye alirudia tena kurudi nyumbani saa 6 usiku, na kutoroka shule, kiukweli tumejaribu sana ila ndiyo hivyo tumeshindwa, sasa hv ndiyo yupo kidato cha nne ila hamna hata siku moja anakaa nyumbani kujisomea, amebembelezwa imeshindikana yaani ilifika kipindi akapewa hadi simu ili atulie ila ilipita muda tu akarudia, wikii hii hajaenda shule hata siku moja baada ya kufwatiliwa alikutwa mtoni anavuta bangi na wapo na wenzake wanapasua mawe ya kuuza, kinachoshangaza kila kitu anapata nyumbani. Malipo yote alisha lipiwa, sasa sijui tufanyaje tumekwama tunaomba ushauri wenu wakuu.