Ametenda kosa gani kisheria? Na adhabu ya kosa hilo ni ipi?

Ametenda kosa gani kisheria? Na adhabu ya kosa hilo ni ipi?

Mbavu za Mbwa

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2011
Posts
303
Reaction score
154
Tangu kuzaliwa kwake, anajulikana kwa jina la Issa K. Busotwa. Wakati Wa mtihani Wa kidato cha nne mwaka 2010 alishikwa na mtihani akiwa ndani ya chumba cha mtihani na siku ya mwisho, matokeo yake yalifutwa na Baraza la mtihani la taifa.

Mwaka mmoja baadae, Issa K. Busolwa akaanza kusoma kidato cha nne, na hapa ndipo alipobadili jina kutoka Issa K.Busolwa hadi Issa K.Madunda na vyeti vyake vyote vya masomo na kitaaluma vinasomeka kwa jina la Issa K.Madunda.

In short, cheti cha la saba kinasomeka Issa K. Busolwa na vilivyofuatia (Cheti cha kidato cha nne, sita, Chuo vinasomeka Issa K.Madunda

Pamoja na kuwa na majina tofauti, lakini huyo ni mtu mmoja, tofauti ni Surname tu.

Wakuu, hapo ndugu huyu atakuwa ametenda kosa gani na ktk sheria? Adhabu inayoambatana na kosa hilo ni ipi?
 
Hakuna kosa hapo watumishi wa umma hawakaguliwi vyeti
[HASHTAG]#Bashite[/HASHTAG]
 
Kisheria hao ni wa2 wawili tofauti mpaka akaape kuwa majina yote ni yake
 
Hana kosa,akachukue deed poll kwa mwana Sheria au mahakamani.
 
Back
Top Bottom