Amina Morio Kinabo: Muasisi wa TANU Moshi na mpigania uhuru

Amina Morio Kinabo: Muasisi wa TANU Moshi na mpigania uhuru

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Hakuna kitu hunipa furaha kama niandikapo historia ya mtu kisha akatokea msomaji akaniandikia kuniambia huyo uliyemtaja ni babu au bibi yangu.

Hivi karibuni niliandikiwa na Adam Ahmed kuhusu nyumba aliyolala Mwalimu Nyerere Mikindani safari yake ya kwanza Southern Province mwaka wa 1955 baada ya kutoka UNO.

Aliniandikia na kuniletea picha ya nyumba ile ya ghorofa moja kama ilivyo sasa.

Nyumba hii aliyolala Mwalimu ilikuwa nyumba ya babu yake.

Kiasi cha kama mwezi mmoja niliandika jina la Bi. Amina Kinabo na mjukuu wake Idd Twaha Lema akasoma makala ile.

Bwana Idd kaniandikia na kaniletea picha nyingi za bibi yake Bi. Amina Kinabo wakati wa uhai wake baada ya uhuru akishughulika na harakati za ujenzi wa taifa.

Pamoja na picha kaniletea pia nyaraka za TANU Tawi la Moshi Mjini wakati wa kupigania uhuru.

Angalia barua kutoka maktaba ya Bi. Amina Kinabo kuhusu ziara ya President wa TANJ Julius Nyerere Northern Province mwaka wa 1957.

Siku zote nikisononeka kwa kukosa picha tatu za wanawake shujaa wa Kilimanjaro waliopigania uhuru wa Tanganyika - Bi. Amina Kinabo, Halima Selengia na Mama bint Maalim.

Mzee Yusuf Olotu aliyenifundisha historia ya TANU Moshi mjini anasema TANU Moshi ilijengwa kwa juhudi za akina mama kwa uanachama na kwa fedha zao.

Nilihangaika kupata picha za akina mama hawa bila mafanikio.

Hivi mpaka lini tutaendelea kuipuuza historia ya mashujaa wetu?

Screenshot_20201106-061246.jpg

Bi. Amina Kinabo

Screenshot_20201106-064536.jpg
Screenshot_20201106-064855.jpg
 
Namfahamu Bi Mkubwa huyu kwa sababu nilipata bahati ya kumuona yeye na hata mwanae Alhaj Twaha Lema miaka ya 1980s akiwa ameshakua mtu mzima wakati huo tukimuita Mama Morio. Alikua ni mtu madhubuti sana mwenye kuheshimika na marehemu mwanae, al marhumu Alhaj Twaha Lema aliishi katika kitongoji cha Pasua kilichopo nje kidogo ya Moshi Mjini katika nyumba inayotazamana na Shule ya Msingi Pasua( sina hakika kama shule na nyumba bado vipo)

Hii ni familia maarufu sana na Alhaj Twaha Lema ni miongoni mwa mahujaji wachache kutokea Kilimanjaro waliobahatika kwenda Hija miaka ile. Wakati huo ni watu wachache sana hasa kama ni pembezoni mwa mji waliweza kumiliki simu za mezani zile za Shirika la Posta na Simu na Mzee Lema alikua miongoni mwao huku watu wa kitongoji cha Pasua maranyingi wakienda kupokea simu zao kutoka mbali kwenye nyumba ya Alhaj
 
kumbe kuna wachaga waislamu?
KITABU KIPYA: UISLAM ULIVYOINGIA UCHAGGANI

Rajabu Ibrahim Kirama alikuwa mtoto mdogo wakati Wamishionari wanaingia Kilimanjaro baada ya Mkutano wa Berlin mwaka wa 1884 na Wajerumani wakaingia Uchaggani kuanza kutangaza Injili wakati huo jina alilopewa na baba yake lilikuwa Kirama Mboyo.

Baba yake aliyejulikana kwa jina la Muro Mboyo alikuwa Jemadari wa Majeshi ya Mangi Ndeseruo Mamkinga wa Machame.

Sintofahamu baina ya Mangi na Jemadari wake ulisababisha Jemadari Muro Mboyo kwenda kuishi uhamishoni Old Moshi kwa Mangi Rindi Mandara na mkewe aliyekuwa anaitwa Makshani Olotu kurudi kwa wazazi wake Kibosho kwa Mangi Sina akiwa na mwanae mdogo Kirama.

Huyu mtoto mdogo Kirama alipokuwa mtu mzima aliuingiza Uislam Uislam Machame.

Mama yake Makshani bahati mbaya hakuupokea Uislam lakini baba yake aliporudi Machame wakati wa utawala wa Waingereza yeye alitoa shahada na jina alilochagua ni Ibrahim, ''Rafiki wa Allah.''

Kuna mengi aliyopitia Rajabu Ibrahim Kirama katika harakati zake za kuupigania Uislam akipambana na Mangi wa Machame wa wakati ule Abdiel Shangali akizuiwa kujenga msikiti na alipojenga ukavunjwa kwa amri ya Mangi.

Alipambana na Waingereza wakati anataka kujenga Muslim School ya kwanza Uchaggani akinyimwa misaada ya fedha ambayo serikali ilikuwa inatoa kwa shule za Misheni.

Kwa ustadi mkubwa Rajabu Ibrahim Kirama alisafari hadi Zanzibar kutoka msaada kwa Sayyid Khalifa bin Humud na kukutana na Sheikh Hassan bin Ameir na kuweza kuunga udugu na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ya Dar es Salaam na kufungua tawi Machame Nkuu kijijini kwake katika miaka ya 1930.

Historia hii haikamiliki bila kutaja ukoo wa Marua na haikamiliki kamwe bila kuwataja vijana wadogo wanne waliotoka Zanzibar kuja Uchaggani na Upare kusomesha Qur'an - Shariff Allawi, Sheikh Mahmud Mshinda, Sheikh Abdallah Minhaj na Sheikh Saleh Mwamba.

Historia hii imechelewa kuandikwa na ndani ya kitabu hiki mna mafunzo mengi lau yaliyotokea inafika sasa zaidi ya miaka 300 historia hii ikihadithiwa kutoka kizazi hadi kizazi.

Kitabu kipo Ibn Hazm Media Centre In Shaa Allah Manyema, Mtoro, Mtambani na Tanzania Publishing House (TPH).

Bei Shs: 10,000.00
 
KITABU KIPYA: UISLAM ULIVYOINGIA UCHAGGANI

Rajabu Ibrahim Kirama alikuwa mtoto mdogo wakati Wamishionari wanaingia Kilimanjaro baada ya Mkutano wa Berlin mwaka wa 1884 na Wajerumani wakaingia Uchaggani kuanza kutangaza Injili wakati huo jina alilopewa na baba yake lilikuwa Kirama Mboyo.

Baba yake aliyejulikana kwa jina la Muro Mboyo alikuwa Jemadari wa Majeshi ya Mangi Ndeseruo Mamkinga wa Machame.

Sintofahamu baina ya Mangi na Jemadari wake ulisababisha Jemadari Muro Mboyo kwenda kuishi uhamishoni Old Moshi kwa Mangi Rindi Mandara na mkewe aliyekuwa anaitwa Makshani Olotu kurudi kwa wazazi wake Kibosho kwa Mangi Sina akiwa na mwanae mdogo Kirama.

Huyu mtoto mdogo Kirama alipokuwa mtu mzima na akauingiza Uislam Uislam Machame. mama yake Makshani bahati mbaya hakuupokea Uislam lakini baba yake aliporudi Machame wakati wa utawala wa Waingereza yeye alitoa shahada na jina alilochagua ni Ibrahim, ''Rafiki wa Allah.''

Kuna mengi aliyopitia Rajabu Ibrahim Kirama katika harakati zake za kuupigania Uislam akipambana na Mangi wa Machame wa wakati ule Abdiel Shangali akizuiwa kujenga msikiti na alipojenga ukavunjwa kwa amri ya Mangi.

Alipambana na Waingereza wakati anataka kujenga Muslim School ya kwanza Uchaggani akinyimwa misaada ya fedha ambayo serikali ilikuwa inatoa kwa Shule za Misheni.

Kwa ustadi mkubwa Rajabu Ibrahim Kirama alisafari hadi Zanzibar kutoka msaada kwa Sayyid Khalifa bin Humud na kukutana na Sheikh Hassan bin Ameir na kuweza kuunga udugu na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ya Dar es Salaam na kufungua tawi Machame Nkuu kijijini kwake.

Historia hii haikamiliki bila kutaja ukoo wa Marua na haikamiliki kamwe bila kuwataja vijana wadogo wanne waliotoka Zanzibar kuja Uchaggani na Upare kusomesha Qur'an - Shariff Allawi, Sheikh Mahmud Mshinda, Sheikh Abdallah Minhaj na Sheikh Saleh Mwamba.

Historia hii imechelewa kuandikwa na ndani ya kitabu hiki mna mafunzo mengi lau yaliyotokea inafika sasa zaidi ya miaka 300 historia hii ikihadithiwa kutoka kizazi hadi kizazi.

Kitabu kitakuwa Ibn Hazm Media Centre In Shaa Allah Manyema, Mtoro, Mtambani na Tanzania Publishing House (TPH).
Kitabu ni hicho hapo chini:

Screenshot_20201013-170304.jpg
 
Naona bado unapambana kutuonyesha jinsi kina mama wakiislam walivojitoa kwa hali na mali kupigania ukombozi wa nchi lkn wakasahaulika kwa maksudi kabisa.
 
Je huyu ana undugu na mgombea ubunge jimbo la Kibaha vijijini (CHADEMA) Edward Kinabo?
 
Back
Top Bottom