Mzee ES
Kasheshe la Florida lilianza usiku wa siku ya kupiga kura na likaisha siku Mahakama kuu ya Marekani ilipositisha zoezi la kuhesabu kura huko Florida. Mambo ya intimidation, hanging chard, mtu mweusi kunyimwa haki ya kupiga kura, watu wenye umri mkubwa kushindwa kutoboa kitobo cha karatasi, udanganyifu na wizi wa kura, kura kuhesabiwa upya na kokoro zote zilizofuatia, suluhisho lake lilikuwa ni la kisheria tu. Legal wrangling. Umaarufu wa mtu haukuwa na nafasi tena kwa sababu hakukuwepo upigaji kura na kampeni zilisha isha. Mtu aliyekuwa anahitaji msaada Florida alikuwa Gore na siyo Bush.
Katika saga lile, strategy ya Bush ilikuwa ni kuweka watu kwenye ground Florida ili kuhakikisha kura hazihesabiwi tena. Jopo la Bush liliongozwa na James Baker. Strategy ya Gore, ilikuwa kinyume. Alitakiwa kuwa na watu wa kuhakikisha kura zinahesabiwa upya. Jopo la Gore liliongozwa na Wallen Cristopher. Kumbuka Floridas battle haikuwa state nzima. Ilikuwa ni sehemu ambazo ni heavily Democrats ambao ni weusi, masikini, na wazee wengi wao ni wale waliohmia huko mfano jews etc. Sehemu hizo ni Broward, Palm Beach, Miami-Dade, na Volusia counties. Also, remember, one of the most controversial aspects of the Florida election was the so-called butterfly ballot used in heavily Democratic Palm Beach County. Many voters came out of the polls saying they were confused by the ballot design.
Kitendo cha kumpeleka Powel pale ingekuwa ni kutetea haki za weusi na wanyonge. Kumbuka Powel ni Republican, ingawa sera kama za affirmative actions ndizo zilimfikisha pale alipo, hata hivyo, haziamini na hapo ndipo anapotofautiana na Jesse Jackson. Huwezi kumvuta hata kwa mtutu wa bunduki kwenda kutetea weusi wasioenda shule. Powel kwenda kwenye saga la Florida kusingemsaidia Bush hata kidogo. Gore alihitaji msaada wa watu mashuhuri kwenda Florida kushinikiza ili kura zihesabiwe upya. Bush Hakuhitaji mtu mashuhuri kwasababu chombo kilichokuwa na mamlaka ya juu ya kusimamia na kutangaza mshindi Florida kilikuwa kinaongozwa na mwana mama wa Republicans ambaye mwaka huu anagombea usenetor. Pia, Bunge la Florida lilikuwa linaongozwa na Republicans. Jeb Bush ambaye ni gavana wa Florida na ndugu wa Bush, yeye alifanya umafia kabla ya uchaguzi, hivyo kwenye sakata alijifanya kukaa pembeni ili kujihusisha kwake kusilete nongwa (PR). Yeye alijifanya kuwa msimamizi wa sheria na kuangalia mipaka yake ya uongozi. Gore alichokuwa nacho ni Mahakam kuu ya Florida ndiyo imejaa watu waliteuliwa na viongozi wa Democrats
Strategy ya pili ya kambi za Bush na Gore ilikuwa kuhakikisha wamarekani hawachoki kwa sababu sakata lilichukua muda mrefu. Zilikuwepo calculations za public relations (PR). Democrats ni chama kilichojaa watu wanaotetea haki za kila kitu unachokijua wewe duniani. Wote walijipeleka Florida. Wanasheria wengi sana Marekani ni democrats hivyo walipanda ndege na kwenda kujitolea tu. Hata yule mwanasheria aliyebobea wa Marekani bwana David Boies alijitolea bila kulipwa kumwakilisha Gore toka mahakama za rufani za Florida mpaka Mahaka kuu ya Marekani. Republicans wao wanafedha.
Hivyo, kwenye TV kambi zote mbili zilikuwa makini kuhakikisha nani anaongea kwa niaba ya nani? Walimuweka Gore na Bush kwenye TV kwa mahesabu ya juu sana. Pia walichagua watu wa kuongea kipindi fulani na wakati fulani. Walikuwa hawaendi hovyo. Suala muhimu hapa, lilikuwa kuhakikisha inner circle ya Bush na inner circle ya Gore hawatokezi kwenye TV. Waliogopa ku-backfire. Kumbuka kwenye kampeni, kambi ya Bush ilishatoa nyeti makusudi kuwa Powel angekuwa waziri wa masuala ya kigeni. Powel ni mmojawapo wa watu ambao hawakwenda Florida na wala hawakutokea kwenye TV kuongelea chochote kuhusu saga lililokuwa linaendela kule Florida.
Kilichokuwa kinaangaliwa ni sheria za Florida zinasema vipi kuhusu utata wote ule. Powel had nothing to do with state laws. Mahakama ya Florida ya ilipoamua kura zihesabiwe upya ambao of course ulikuwa ni ushindi kwa Gore, Bush akakimbilia Mahakama Kuu ya Marekani ambayo iko juu ya vimahakama vya states zote. Alikwenda kule akijua kuwa uwiano wa majaji walioteuliwa na maraisi wa Republicans ni mkubwa kuzidi wa wale walioteuliwa na maraisi wa Democrats. Ni kweli, Bush alishinda uraisi kwa kura moja ya jaji wa mahaka kuu ambayo matokeo yake yalikuwa 5-4. Kura ziligawanyika kutokana na itikadi za majaji na kwa jinsi wlivyoteuliwa na maraisi wa hivi vyama. Hivi ndivyo uamuzi wa mahaka kuu ya Florida wa every vote counts ulivyotenguliwa.
Kweli kama unavosema kuwa Bush alihitaji msaada in order to heal the country ambayo ilikuwa imegawanyika vibaya sana kutokana na lile sakata lililoanza usiku wa uchaguzi na kuisha tarehe 12 mwezi wa kumi na mbili mwaka 2000, when the U.S. Supreme Court overturned a Florida Supreme Court ruling ordering a full statewide hand recount of all undervotes not yet tallied. Mzee ES kadili nilivyokuelewa unadhani umuhimu wa Powel ulikuja katika kipengele cha kuleta umoja wa taifa lililokuwa limegawanyika. Ni kweli kuwa Bush alimteua Powel ili kuonekana ana reach out. Automatically, hiyo ilitakiwa ku-neutralize uchungu wa Florida. Hata hivyo, kabla ya uchaguzi hakuna aliyejua kuwa mahakama kuu ya Marekani ndiyo itamuweka Bush madarakani.
Ingawa Weusi, Waisrael, na Wazungu wa kima cha chini wanaoishi kwenye maeneo niliyoyataja kule Florida ndiyo walionewa kwenye uchaguzi kwa madai ya kura zao kutokuhesabiwa and all sorts of intimidations, lakini kilichokuwa mezani na kilichogawa nchi ni matokeo ya uchaguzi na nani atakwenda kutekeleza sera na kulinda maslai ya nani. Hivyo, nchi haikugawanyika kati ya weusi na weupe au kima cha chini na matajiri. Nchi iligawanyika kati ya kile wanaita Red states and Blue states (majina ya rangi ilitokana na ramani za kwenye TV). Kwa lugha nyepesi ni liberals and conservatives. Mitizamo ya kulia na kushoto. Ukipenda unaweza kusema Democrats na Republicans. Mfano majimbo kama Texas kumchagua Raisi wa democrat ni sawa na kuandika nane kwenye maji. Au state kama New York kumchagua Raisi wa Republican ni kasheshe kwelikweli.
Bush alijaribu kuazima busara za kuiunganisha nchi iliyokuwa imegawanyika kiitikadi na siyo kirangi. Powel ni Republicans independent thinker ndani ya republican. Kama ulikuwa unataka kutibu kidonda cha democrats, ni sawa na kutia dawa ya chumvi. Utawala wa Clinton ndiyo ulimlazimisha Bush kumtafuta Powel wakati wa Kampeni. Clinton, ukiondoa scandal za wanawake, alikuwa ameiweka nchi ya Marekani katika hali ya kiwango cha juu cha uchumi katika mifuko ya wamarekani. Historia ya wamarekani ni kuwa kama Raisi alifanya kazi nzuri ya kuinua maisha ya wamarekani, basi makamu wake huwa anakuwa na nafasi ya kushinda uraisi. Pia Raisi mwenyewe mara nyingi anashinda awamu ya pili. Ukweli huu huwa unafutwa katika kipindi cha majanga makubwa au nchi ikiwa kwenye vita. Kwa historia tu, Gore alikuwa na nafasi nzuri ya kuiongoza marekani. Watu huwa wanafikiri kuwa makamu wa raisi ataendeleza yale yaliyokuwepo.
Utawala wa Clinton ulimlazimisha vipi Bush kumfuata Powel wakati wa kampenil? Hii ilikuwa muda mrefu kabla ya kupiga kura zilizo zaa saga la Florida. Clinton alikuwa na sera zilizowatetea wanyonge wakiwemo watu weusi. Affirmative action ilitukuzwa kama salamu maria wakati wa Clinton. Hata mfagizi wa Ikulu alikuwa mweusi. Wapishi, wapiga picha, ambosi wa secret service, yule mwana sheria lafiki yake kipenzi Jordan ambako alikuwa anakwenda kupumzika kama unavyosikia Bush anakwenda kupumzika Texas. Clinton hakuwapa vyeo vya juu sana minority, lakini alikuwa na sera zilizowainua kimaisha na wakateuliwa katika nyazifa nyingi throught the country. Unakumbuka hata yule waziri wa mambo ya biashara mweusi ambaye alifia kwenye ajali ya kwenye ndege. Clinton alitoka machozi. Hata wamexicano Clinton alikuwa nao tu. Kama yule ambeye sasa hivi ni gavana wa New Mexico Richardson ambaye inasadikiwa atagombea uraisi mwaka 2008. Wote hao waliingia kwenye ramani ya Marekani kwa sababu ya Clinton
Clinton aliishi na weusi Ikulu na walimfuata sehemu aliko enda. Bush alitaka kupata kura za minority angalau za kutosha. Kumbuka alishinda uraisi kwa kura za Florida kama miasita hivi. Hii ni kadiri ya umamuzi wa mahaka kuu ya Marekni. Pia kumbuka anatoka Texas na alikuwa Gavana. Hakuwa na historia yoyote ya kuwa na minority karibu ingawa Texas wamejaa watu kutoka Mexico. Hata kama alikuwa nao karibu, ni watu matajiri wachache, au wale wasomi kama akina Rice na huyu Attorney General wake ambaye alisomea Rice University na Yale zote moto wa kuotea mbali. Ilimbidi atafute mtu wa kumtetea na kuonyesha kuwa ana reach out.
Mtu huyo alitakiwa apendwe na weusi na apendwe pia na kambi yake Bush. Hakuna mtu zaidi ya Powel. Hata bintie Rice kwa wakati huo asingeweza kuziba lile pengo. Alimtumia Powel kwenye miji iliyojaa weusi kupiga kampeni. Walisimama wote kwenye jukwaa utafikiri Powel ndiye alikuwa anagombea uraisi. Walikuwa Michigan, Pensylovenia, Illinois, na kwingineko. Cha ajabu Powel alikwenda Florida na Bush mara moja kwenye kampeni. Lakini walicheza wote ngoma katika hiyo miji kwa muda wote.
Kwa nini kambi ya Bush ilitoa Leak kwenye vyombo vya habari na Bush mwenyewe akakataa kukanusha au kukubali kuwa Powel atakuwa waziri wake wa masuala ya kigeni kabla ya uchaguzi? Wamarekani wameendelea siyo kama tulivyo sisi. Hata kimawazo weni wao wanaweza gundua janja ya nyani kula mahindi mabichi. Kwa wamarekani weusi, kuwa na rangi nyeusi haimaanishi wewe ni mweusi. You just black in color but not black American. Hakuna mtu mweusi kama Clarence Thomas, a US Supreme court justice. (nawashangaa na ubaguzi wetu, hawa majaji ndiyo waliomuweka Bush madarakani). Huyu jamaa ni mweusi kama mkaa. Hata hivyo, kamuulize mmarekani mweusi yeyote yule. Au kaongee na Maya Angelo, Oprah ma wengineo manake nikisema kamuulize Jesse Jackson utadhani nimevuka mipaka. Hawaamini kuwa ni Mmarekani mweusi hata kidogo. Na yeye anajua. Mtangazaji maarufu wa redio za conservative huko marekani bwana Rush Limbaugh ambaye ni mbaguzi kupindukia. Aliwahi kutangaza kuwa Wamarekani weusi wametoka utumwani mpaka Ikulu. Anaamini kuwa Clinton ni Mmarekani mweusi. Ni kweli, huwezi kuwashawishi weusi wa Marekani kuwa Clinton ni mzungu. Wanaamini kuwa Clinton ni mweusi mwenzao. Hata wazungu wanaamini hivyo. Ndiyo maana walifanya mikasa yote ili kumuondoa pale Ikulu. Kwenye kampeni za uchaguzi 2000, Bush alikuwa na slogan kuwa we will bring the integrity to the white house. Watu walidhani anaongelea mambo ya kuchombeza ya Monica. Hapana! Ilikuwa kuwaondoa weusi wote waliokuwa wanafanya kazi Ikulu akiwemo Clinton mwenyewe na kutokubakiza makombo ya akina Gore. Wazungu walikuwa wanaelewa anaongelea nini.
Hivi ndivyo Powel aliingia kumsaidia Bush. Kambi ya Bush walitaka kuonyesha kuwa watamchagua mweusi kushika madaraka makubwa kuliko alivyofanya Clinton na yatakuwa madaraka ya kwanza kufikiwa na mwafrika. Walipingwa na kambi ya Gore kwa kueleza kuwa weusi sio kushika madaraka na kusimamia sera za ukandamizaji. Weusi siyo rangi, bali ni maisha, utamaduni na historia. Walimpenyeza Jesse Jackson kufanya kazi hiyo. Ni kweli kambi ya Gore ilifanikiwa kwa hilo kwani Bush alipata asilimia ndogo ya kura za weusi na ndiyo maana hatambui jumuia zao na hata wakimualika huwa haendi kinyume na maraisi waliopita. Aliposhinda, kwasababu kampeni yake ilishamshikia kidedea Powel, hakuwa na chaguo ila kutimiza zile fununu zilizokuwa zimetapakaa na hata siku moja kule Michigan aliwahi kueleza kwenye jukwaa kuwa mnmuona huyu, hawa ndiyo viongozi tunowataka. Alikuwa anajibu hoja za kambi ya Gore kuwa tunataka sera na viongozi wanaofanana na Marekani (nchi ya mchanganyiko).