Umeshasema kwamba askari walikua wanatoa heshima kwa mgeni rasmi....sasa swali lako la nn tena?Jan, tar. 12 tulishuhudia askari wetu wakipita mbele ya mgeni rasmi Mh. Karume wakitoa heshima kwa mkuu. Lakini Mh. mwingine ambaye ni Rais wa jamhuri ya Muungano wa TZ alikuwepo.
Mpaka leo sipati jibu kuhusu amiri jeshi mkuu ninani? na kwanini Mh. wa Zanzibar ndiye alikuwa mkuu, wakati mkuu kabisa alikuwepo? au labda hivi vyeo ni vya kupokezana kwa muda? Wataalam wa protokali tueleweshe.
Inawezekana hicho cheo hakimo kwenye mambo ya muungano.
hata mie niliwaza hivyo mwanzoni, kuwa jamaa alikua mkekani akisubiri pilau kwa biliani na soda bariiidi.....usikute amirijeshi mkuu alikuwa kwenye hitima akamuagiza amuwakilishe
Heshima kwenu wanajamvi,
Amiri jeshi mkuu wa Tanzania ni Rais wa JMT ambae ni Jakaya Mrisho Kikwete.Binafsi nilistuka sana kuona mkuu wa nchi [JMT] anakaa jukwaa na Bwana mdogo Karume anapewa kiapo cha utii.
Hizi sarakasi zilianza tangu enzi za komando Salmin Amour akiwa Rais wa Zanzibar sasa yamekuwa mazoea tu.Sijui kama kumbukumbu zangu ziko sahihi protokal haikuzingatiwa hata wakati waheshimiwa walipokuwa wanaingia uwanjani na wakati walipokuwa wanatoka.Kawaida Rais anatakiwa awe mtu wa mwisho kuingia kiwanjani,na anakuwa mtu wa kwanza kuondoka kiwanjani lakini hili nalo niliona limegeuzwa kabisa Karume ndiye aliyekuwa wa mwishi kuingia na wa kwanza kuondoka kiwanjani.
Hakuna Cheo cha Amiri Jeshi Mkuu Msaidizi Tanzania!!!Ngoja nijaribu na kujaribu sio kushindwa
Amiri Jeshi Mkuu J .M. K
Amiri Jeshi Mkuu Msaidizi A .A. K
Ila nadhani sasa imefika muda KATIBA yetu sasa ijadiliwe upya mikanganyiko kibao jamani
Wana JF,Nashukuru kwa comments zenu. Kumbe tuko wengi tunao kosa majibu ya swali hili. Labda mhusika wa hii blog atusaidie kui- 'forwad kwa wataalam kama akina Dr. Sira napengine tuikuze ili itusaidie tumpe live mhusika siku nyingine awe makini na mambo ya kiitifaki, pia kukumbushana kulinda Katiba yetu.
tatizo ni uzingatifu wa protokali, siyo kukagua tuKukagua jeshi tu mbona simple sana, hata Masha waziri wa mambo ya ndani huwa anakagua Gwaride la Polisi. Mi naona hapo wanachukulia vitu simple tu bila kujali umuhimu wake katika katiba.
Jan, tar. 12 tulishuhudia askari wetu wakipita mbele ya mgeni rasmi Mh. Karume wakitoa heshima kwa mkuu. Lakini Mh. mwingine ambaye ni Rais wa jamhuri ya Muungano wa TZ alikuwepo.
Mpaka leo sipati jibu kuhusu amiri jeshi mkuu ninani? na kwanini Mh. wa Zanzibar ndiye alikuwa mkuu, wakati mkuu kabisa alikuwepo? au labda hivi vyeo ni vya kupokezana kwa muda? Wataalam wa protokali tueleweshe.