Amiri Jeshi mkuu wa Tz ni nani?



Mheshimiwa Dr. Slaa,

Nikushukuru kwa mchango wako madhubuti, unaonyesha kwa undani kiini migogoro inayoletwa na katiba yetu. Ni jambo la kusikitisha kwamba Bunge letu linashindwa kuyatatua haya matatizo na kutaka kuvirisisha vizazi vijavyo matatizo. Swali la kujiuliza , je muungano wetu utaweza kudumishwa ndani ya hii katiba? Na jee, when everything is set and done, nyie wabunge mtakumbukwa kwa kitu gani ?

Ni jambo la kusikitisha sana kwamba Tanzania sasa inakimbilia kuanzisha East Africa Federation wakati tumeshidwa kutatua matatizo ya Muungano wetu huu. Tumekuwa wepesi sana wa kukimbilia mambo bila ya kuyafanya uchunguzi yakinifu ! Katiba iliyopo sasa haitaweza kuulinda huu muungano na hatima yake utakufa, kama ambavyo muungano wa East Africa utakavyokufa pia ...
 
Ngoja nijaribu na kujaribu sio kushindwa

Amiri Jeshi Mkuu J .M. K
Amiri Jeshi Mkuu Msaidizi A .A. K

Ila nadhani sasa imefika muda KATIBA yetu sasa ijadiliwe upya mikanganyiko kibao jamani

kama ni kujaribu umeangukia pua hapo A A K hayumo. Makamu wa rais ndiye rasmi na kama hayupo manyota lazima awe spika wa bunge la JMT
 
Inabidi watu wa kitengo cha Itifaki cha wizara ya mambo ya nje itupe ufafanuzi zaidi coz ndo wahusika wenyewe.
 
Rufiji,
Asante kwa maswali na hoja yako nzuri.
i) Kwanza, kwa taratibu za kawaida na kwa Sheria na Kanuni za Bunge, Serikali ndiyo inayowasilisha Miswada, bajeti ndani ya Bunge. Serikali ya Chama kilichoshinda ndiyo inayotekeleza Sera inayokuwa dira ya kuongoza nchi kutokana na Ilani( na Sera) ya chama kilichoshinda uchaguzi. Kanuni za Bunge Toleo la 2007 inatambua sasa Hoja, na Miswada ya Wabunge au mmoja mmoja au kama Kamati. Lakini kwa uzoefu, hoja na miswada ya namna hiyo haijawahi kufanikiwa kwa kuwa hutekwa na Serikali, na kisha huziacha bila kufanyia kazi. Mfano ni Mswada binafsi wa Mhe. Zitto Kabwe kuhusu Maadili ya Viongozi, ambao ulitimiza masharti yote, ukapokelewa na Ofisi ya Katibu wa Bunge, lakini kwa sababu zisizojulikana ukapelekwa Serikalini na haujarudi hadi leo na Bunge linaisha sasa. Hivyo, ni sahihi kusema kuwa kwa uzoefu wa Bunge letu, ni Miswada ya Serikali tu ndiyo inayofanyiwa kazi na Bunge.
2) Utaratibu wa marekebisho ya Katiba ni mlolongo mrefu. Marekebisho hayo nayo huletwa na Serikali. Wabunge, kimsingi wanapitisha kinacholetwa na Serikali, na kwa kiwango fulani kukifanyia marekebisho, tena iwapo Waziri husika atakubali.
3) Mfumo wa Bunge letu, ni kuwa zaidi ya asilimia 80 ya Wabunge wanatoka Chama Tawala. Hawa hupitisha kila kitu kinachotoka kwenye Serikali yao. Mfano halisi ni mjadala wa Richmond, ambao kimsingi ulifungwa kwa matakwa ya Chama chao. Hivyo, kwa mfumo wa Sasa huwezi kuwalaumu wabunge wote, katika ujumla wao, labda, tuwalaumu Watanzania ambao huwa wanachagua Wabunge kutoka Chama kimoja na hivyo kutengeneza kitu kinachofanana na " Dictatorship of one Party in the Parliament". Kwa mfumo huo tusitegemee mabadiliko yeyote ya maana, hadi Watanzania katia umoja wao watakapoamua kufanya mabadiliko ya msingi saa. Natumaini hoja inaeleweka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…