Amissi Tambwe wa Yanga na rekodi ya ajabu TAIFA

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
Straika wa Yanga, raia wa Burundi, Amissi Tambwe, ameweka bonge la rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kupiga hat-trick (mabao matatu mechi moja) tatu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mrundi huyo, ni mchezaji pekee aliyeweka rekodi hiyo ambayo haijawahi kuwekwa na mchezaji yeyote tangu uwanja huo ulipoanza kutumika.

Tambwe, mechi yake ya kwanza kufunga hat trick kwenye uwanja huo ilikuwa ni Februari Mosi, 2014 dhidi ya JKT Oljoro akiwa na Simba ambayo ilishinda 4-0.

Mechi nyingine ambayo Mrundi huyo alifunga hat trick ilikuwa ni Septemba 19, 2014 dhidi ya Mgambo JKT ambayo timu yake ya Simba ilipata ushindi mnono wa mabao 6-0.

Mshambuliaji huyo alikamilisha rekodi yake ya kupiga hat-trick ya tatu wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa kwa kufunga mabao manne katika ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Coastal Union iliyocheza na Yanga.

Tambwe aliyekuwa mfungaji bora msimu uliopita wa ligi kuu akifunga mabao 19, alitua kuichezea Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea Simba baada ya kumsitishia mkataba wake kabla ya kutua Jangwani.

Upo uwezekano mkubwa wa mshambuliaji huyo kukitetea kiatu chake cha dhahabu kutokana na kasi yake kubwa aliyonayo hivi sasa ya kufunga mabao.

Mrundi huyo, hadi hivi sasa amefanikiwa kufunga mabao 9, akiongozwa na Simon Msuva mwenye 13 akifuatiwa na mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu aliyepachika 10 na Rashid Mandawa wa Kagera Sugar ambaye naye ana mabao 10.


Kati ya hat-trick hizo alizozipiga, idadi kubwa ya mabao amefunga kwa kichwa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufunga aina hiyo ya mabao huku mengine kwa
 

Attachments

  • images-2.jpeg
    6.4 KB · Views: 366
  • images.jpeg
    10.3 KB · Views: 189
  • images-4.jpeg
    12.5 KB · Views: 170
  • images-5.jpeg
    14.3 KB · Views: 365
  • images-1.jpeg
    10.1 KB · Views: 190
Mungu kamjaalia kichwa kikubwa, naye bila ajizi anakitumia vizuri kuwatesa magolikipa.

Asanteni Simba kwa kumtema, sisi ametufaa sana hadi na ninyi mnamtamani tena.
 
Mungu kamjaalia kichwa kikubwa, naye bila ajizi anakitumia vizuri kuwatesa magolikipa.

Asanteni Simba kwa kumtema, sisi ametufaa sana hadi na ninyi mnamtamani tena.
Simba bwana wanachekesha kweli wamemuacha mchezaji wa mpira Amiss Tambwe magoli wakamsajili msanii wa muziki Danny Serunkuma "Mpoto".
Hongera sana Amiss Tambwe kwa kuweka record ya kipekee katika misimu yako miwili ya kulichezea soka la kibongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…