“Ammunition Hill/Operation Opera” Tukio Lingine la kumuwahi Adui Kwa kumpiga Ngumi ya Chembe(Mossad)

“Ammunition Hill/Operation Opera” Tukio Lingine la kumuwahi Adui Kwa kumpiga Ngumi ya Chembe(Mossad)

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Miaka 35 baada ya operation opera … ambapo majeshi ya Israel yalishambulia na kuteketeza kinu cha saddam Hussein cha kufulia nyuklia huko Osirak. Mwanajesh mstaafu wa IAF na MOSSAD anaamua kuweka wazi habari ambazo zilikuwa ni za siri miaka hiyo. Ofisa huyu wa mossad anasimulia tukio hilo ambalo pia pinafahamika kama operation siku ya ijumaa

Jeshi la anga la Israel lilipata habari kupitia wapelelezi wake mahiri kuwa Saddam Hussein alikuwa ana vinu vyenye uwezo wa kutengeza nyuklia kitu ambacho kilikuwa kinatishia usalama wa taifa la Israel.

Katika kufunua mambo hayo kituo cha tv cha channel 10 Col Zeev Raz ambaye aliongoza shambulio hilo la tarehe 7 june mwaka 1981 anasema jesh la anga na wataalamu wake waligundua kuwa kwenda Iraq na kurudi umbali wa mile 2000 (km 3218) lilikuwa jambo gumu sana kutokana na huo umbali kwa kutumia jet zao. Hivyo wakaamua kufanya manuva na ujanja mwingine ili kuweza kuwezesha jambo hilo kutendeka. Waliitwa wataalam wa hesabu na Fizikia wa mambo ya mashine za kijeshi wafanye mchakato kuwa jambo hilo linafanikishwa vipi.

Jeshi la Israel lisingeweza kutegemea ndege za usa ambazo zilikuwa na uwezo mdogo wa kujaza mafuta kwenye hizo jets kwa wakati huo.na katika kulifanikisha hilo waligundua kuwa hilo jambo lingechukua muda mpaka mwaka 1982 ambapo intelejensia ilipofanya kazi yake ya upembuzi yakinifu ikaona kuwa muda huo vinu hivyo vitakuwa vimekamilika ujenzi na hivyo kuwa hatari kwao.

Hivyo shambulio halikupaswa kucheleweshwa maana waswahili wanasema “chelewa chelewa utamkuta mtoto si wako” au "Ukichelea mwana Kulia utalia wewe" basi wataalam wakakaa wakiwaza na kuwazua namna gani waweze fanikisha shambulio hilo na mwishowe wakaja na ufumbuzi. Ndege zote za F-16As zilienda na kurudi salama na waliendelea kuficha hiyo siri ziliendaje na kurudi salama. hawakutaka kuielezea dunia walifanya utaalam gani katika jambo hili. kuna siri huwa zinabaki za kijeshi miaka yote na katika hili Israel hufanya mambo against the odds/ against all odds. ukiangalia pia uzi wa Six Day War walifanya utundu kama huu yaani wa Ku improvise.

Kwanza operation ilitwa Ammunition Hill lakin baadaye Waziri mkuu Menachem ambaye alikuwa kiongoz wa Operation hiyo aligundua kuwa kiongozi wa Upinzani Shimon Peres alikuwa anafaham kuhusiana na operation hiyo hivyo akaamua kuisitisha. Maana alitaka iwe siri kabisa. na wenzetu huwa wakitaka kitu kiwe siri kinakuwa siri kweli kweli. si mke si nani anayejua kinachoendelea kwa kuepuka kuvuja kwa taarifa za kiintelejensia.

Osirak-305x172.jpg

Kinu cha kutengeneza Nyuklia Huko Osirak Iraq kabla ya Kulipuliwa na Majeshi ya Israel mwaka 1981

Hivyo wakaamua kuandika operation command kwa jina lingine wakiweka neno Opera. Hili ni neno ambalo lilichaguliwa tu randomly na computer. Anasimulia Major General Davi Ivry aliyekuwa Commander wa IAF. Anasema kuwa harakati za Iraq kujenga vinu vya nyuklia mara ya kwanza iligundulika mwaka 1976 mpaka 1977.

Gad Shimron ambaye alikuwa ni ajent wa Mossad anasema kuwa miaka hiyo Israel walikuwa na watu wao ambao walikuwa wakiwapa taarifa kuhusiana na mipango hiyo ya Iraq kuunda mabomu ya nyuklia wakinunua vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa vinu hivyo. Hivyo hatua za mwanzo zilikuwa ni kuchelewesha uundwaji wa mitambo hiyo halafu baadaye waangalie kama kweli baada ya kuwa vimekamilishwa vinu hivyo vilikuwa na teknolojia ya kutosha kuweza kuzalisha Plutonium.

Shimron anasema Mossad walikusanya kiasi kikubwa sana cha taarifa kuhusiana na ujenzi huo wa vinu vya kinyuklia vya osirak. Anasema kuwa katika hili “mtu hukuhitaj kuwa mtaalam wa kijasusi kugundua kuwa kuna mradi uliokuwa ukiendelea huko Iraq na wakiwepo wataaalam lukuki wa kigeni basi ni wazi tu kuwa mashirika ya kijasusi pinzani yangetaka kujua ni nini kinaendelea “ hivyo hilo suala likaendelea kuwa linafanyika pasipo mtu mwingine yeyote kujua kuwa kuna jasus/majasus ndani ya wale wataalam wakitoa habari kwa Israel. Hivyo mossad wakaanza kwanza na mkakati wa kuchelewesha ujengwaji wa vinu hivyo kwa miaka miwili na nusu. Hivyo kwa kutumia taarifa walizokuwa wanazipata kutoka mossad jeshi la Israel likawa linafanya mikakati namna gani ya kwenda kulipua vinu hivyo kabla havijakamilika. Na hili waliliwaza baada ya kuona ni kweli Iraq walikuwa na uwezo wa kuzalisha madini ya plutonium.

Ilan ramon huyu alikuwa amepewa jukumu la kuandaa raman na kuangalia kama jets IAF zingeweza kwenda na kurudi salama. Ivry aliamini kuwa Jets zingeweza kwenda kirahis na kulipua maeneo lengwa ila shida ilikuwa kurudi salama. Kutokana na umbali na teknolojia ya miaka hiyo ilikuwa ni shida kwenda na kurudi kwa umbali huo pasipo kujaza mafuta.
1280px-IAF_F-16A_Netz_243_CIAF_2004-305x172.jpg

C:\Users\HAPPYD~1\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.jpg


Hii ni ndege ya Israel F-16A Netz 243 ambayo ailiendeshwa na Kanal Ilan Ramon katika operation Opera kwenda kulipua vinu vya nyuklia vya saddam huko Osirak mwaka 1981.

Arye Naor anasema kuwa waziri Mkuu alikuwa amedhamiria kulipua vinu hivyo kwa hali yoyote hata kama kwa kitendo hicho ndo ingekuwa mwisho wa uwaziri wake mkuu. ilikuwa iwe isiwe lazima atimize lengo hilo afe beki, afe kipa.

Upembuzi ukafanyika kuwa inawezekana jet moja au mbili zisiweze kurudi. Hivyo katika kujiandaa na shambulio hilo pilots wakaelekezwa kuwa wamejiandaa ikitokea wakashindwa kurudi au wakakwama huko basi watumie pesa za Iraq ambazo walikabidhiwa ili waweze kutoroka kutoka huko wakiwa ardhini. waliandaliwa katika mazingira yote na ikiwa kama wangetokea wameshindwa kabisa kutoroka basi wasikubali kutekwa wakiwa hai. lilikuwa ni suala la kitaifa zaidi kuliko la mtu binafsi. marubani wote walikubali kwa nia moja maana waliambiwa kwa ambaye hayupo tayari anaruhusiwa kujitoa na wala hatashtakiwa au kufukuzwa kazi.isipokuwa tu atawekwa kwanza chini ya ulinzi mkali mpaka litakapofanyika tukio hilo then aachiwe kuendelea na maisha yake ili kulinda siri. wanajeshi wote walisema wapo tayari kulinda taifa lao kwa gharama yoyote ile.

Baada ya kuwa mara ya kwanza waliahirisha operation hiyo wakaamua kuwa safari hii iwe Jumapili kwa sababu wataalamu wa Nyuklia wa Kutoka UFaransa watakuwa mapumziko. Na wakaambiwa kuwa waepuke mapigano ya uso kwa uso(dog fight) na ndege za Iraq ambazo walikuwa wamenunua Usoviet MiG ikiwa kulikuwa na ndege ya abiria maeneo karibu ili wasilipue ndege hizo na kusababisha vifo kwa wataalamu wa mataifa mengine hivyo kuibua mzozo. Kumbuka hapa kulikuwa pia kuna mambo ya kidiplomasia.

Hivyo ikapangwa safari ambayo haitakuwa mbali sana na zinapopita ndege za abiria za Iraq. Kitaalamu lengo lilikuwa ni kama kuji disguise na kutowapa mashaka wanajeshi wa Iraq. Ndege za kijeshi za Israel ziliingia Iraq pasipo kutambuliwa na majeshi ya anga ya Iraq. Wakapiga vituo hivyo na kuviharibu kabisa. Iraq walipokuja kugutuka walikuwa wameshachelewa ilikuwa ni kama kufumba na kufumbua vituo vile vimelipuliwa na ndege za Israel ambazo mwanajeshi mmoja wa Iraq alishindwa kujizuia shauku yake na kujikuta akiropoka tena kwa mshangao mkubwa sana kuwa zile ndege na marubani wake walikuwa ni Ghost hakuna binadamu ambao wangefanya vile (kitu kilichosababisha auawe na utawala wa saddam maana alionekana kuwa ame appreciate utaalam uliotumika kuja kuwashambulia nchini mwao)

Moshe Melnick ambaye alikuwa akiongoza Mawasiliano muda huo na marubani waliokuwa wakiendesha jets za mashambulizi aliwaambia kuwa mara wamalizapo tukio wakiwa wanarudi ndipo waweze kuwasiliana na makao makuu kutoa taarifa kuwa wapo salama salimini.israel hawakutaka kupoteza ndege wala mtu mmoja katika tukio hilo.

Anasema anakumbuka alikuwa Ilan Ramon ambaye alichelewea kutoa taarifa alipopiga simu na kukawa na kimya kirefu sana. Wote wakapatwa na mashaka lakini katikati ya mashaka hayo alisikika Ramon akisema kwa sauti ya utulivu kuwa he is safe and sound.salama salimini.

Kitendo kile cha kulipua vile vinu kililaaniwa na mtaifa mengi duniani ufaransa wakikasirika sana sababu walitumia pesa nyingi sana ktika ule ujenzi na wataalam wao pia walikuwepo. Lakini Ivry anakumbuka mwaka 1991 aliyekuwa secretary wa USA Dick Cheney alimpa picha ya black and white kutoka angani ikionesha majengo yaliyoharibiwa na akisema kuwa “ mlirahisisha sana kazi yetu”

Akiwa anatoa tamko waziri mkuu akaanza kwa kusema kuwa operation ya kulipua vinu vya kinyuklia vya Iraq imefanikiwa sana . na uamuzi wa kulipua ulichukua miezi mingi iliyopita ukiwa na vikwazo vingi tulifikiria kwa kina na kuamua kuwa mwishoni hatukuwa na uchaguzi mwingine kwa sababu kama tungeshindwa kuamua kutenda sasa basi baadaye ingekuwa tumechelewa sana.

Israel wakaendelea kwa miaka mingi kutangulia mbele ya maadui yao na kufanya kuwa moja ya taifa lenye kuzungukwa na maadui wengi na lenye kuwa na intelejensia ya hali ya juu duniani. Kila mwananchi wa Israel ufahamu kuwa ni wmanajeshi wa akiba kwa maana siku ikipigwa tu filimbi ajikusanye kujiandaa na vita yupo standby. Wakati huo huo mossad wametapakaa dunia nzima wakiwa katika sura tofaut tofaut kama waarabu,waafrika wazungu,wachina,wahindi,wajapan n.k
 
Miaka 35 baada ya operation opera … ambapo majeshi ya Israel yalishambulia na kutekteza kinu cha saddam Hussein cha kufulia nyuklia huko osirak. Mwanajesh mstaafu wa IAF na MOSSAD anaamua kuweka wazi habari ambazo zilikuwa ni za siri miaka hiyo. Ofisa huyu wa mossad anasimulia tukio hilo ambalo pia pinafahamika kama operation siku ya ijumaa

Jeshi la anga la Israel lilipata habari kupitia wapelelezi wake mahiri kuwa Saddam Hussein alikuwa ana vinu vyenye uwezo wa kutengeza nyuklia kitu ambacho kilikuwa kinatishia usalama wa taifa la Israel.

Katika kufunua mambo hayo kituo cha tv cha channel 10 col zeev raz ambaye aliongoza shambulio hilo la tarehe 7 june mwaka 1981 anasema jesh la anga na wataalamu wake waligundua kuwa kwenda Iraq na kurudi umbali wa mile 2000 (km 3218) lilikuwa jambo gumu sana kutokana na huo umbali kwa kutumia jet zao. Hivyo wakaamua kufanya manuva na ujanja mwingine ili kuweza kuwezesha jambo hilo kutendeka.

Jeshi la Israel lisingeweza kutegemea ndege za usa ambazo zilikuwa na uwezo wa kujaza mafuta kwenye hizo jets kwa wakati huo.na katika kulifanikisha hilo waligundua kuwa hilo jambo lingechukua muda mpaka mwaka 1982 ambapo intelejensia ilipofanya kazi yake ya upembuzi yakinifu ikaona kuwa muda huo vinu hivyo vitakuwa vimekamilika ujenzi na hivyo kuwa hatari kwao.

Hivyo shambulio halikupaswa kucheleweshwa maana waswahili wanasema “chelewa chelewa utamkuta mtoto si wako” basi wataalam wakakaa wakiwaza na kuwazua namna gani waweze fanikisha shambulio hilo na mwishowe wakaja na ufumbuzi. Ndege zote za F-16As zilienda na kurudi salama na waliendelea kuficha hiyo siri ziliendaje na kurudi salama.

Kwanza operation ilitwa Ammunition Hill lakin baadaye Waziri mkuu Menachem aligundua ambaye alikuwa kiongoz wa Operation hiyo aligundua kuwa kiongozi wa Upinzani Shimon Peres alikuwa anafaham kuhusiana na operation hiyo hivyo akaamua kuisitisha. Maana alitaka iwe siri kabisa.

Hivyo wakaamua kuandika operation command kwa jina lingine wakiweka neno Opera. Hili ni neno ambalo lilichaguliwa tu randomly na computer. Anasimulia Major General Davi Ivry aliyekuwa Commander wa IAF. Anasema kuwa harakati za Iraq kujenga vinu vya nyuklia mara ya kwanza iligundulika mwaka 1976 mpaka 1977.

Gad Shimron ambaye alikuwa ni ajent wa Mossad anasema kuwa miaka hiyo Israel walikuwa na watu wao ambao walikuwa wakiwapa taarifa kuhusiana na mipango hiyo ya Iraq kuunda mabomu ya nyuklia wakinunua vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa vinu hivyo. Hivyo hatua za mwanzo zilikuwa ni kuchelewesha uundwaji wa mitambo hiyo halafu baadaye waangalie kama kweli baada ya kuwa vimekamilishwa vinu hivyo vilikuwa na teknolojia ya kutosha kuweza kuzalisha Plutonium.

Shimron anasema Mossad walikusanya kiasi kikubwa sana cha taarifa kuhusiana na ujenzi huo wa vinu vya kinyuklia vya osirak. Anasema kuwa katika hili “mtu hukuhitaj kuwa mtaalam wa kijasusi kugundua kuwa kama kuna mradi uliekuwa ukiendelea Iraq na wakiwepo wataaalam lukuki wa kigeni basi ni wazi tu kuwa mashirika ya kijasusi pinzani yatataka kujua ni nini kinaendelea “ hivyo hilo suala likaendelea kuwa linafanyika pasipo mtu mwingine yeyote kujua kuwa kuna jasus alikuwa mmoaja ya wale wataalam akitoa habari kwa Israel. Hivyo mossad wakaanza kwanz ana mkakati wa kuchelewesha uujengwaji wa vinu hivyo kwa miaka miwili na nusu. Hivyo kwa kutumia taarifa walizokuwa wanazipata kutoka mossad jeshi la Israel likawa linafanya mikakati namna gani ya kwenda kulipua vinu hivyo kabla havijakamilika. Na hili waliliwaza baada ya kuona ni kweli Iraq walikuwa na uwezo wa kuzalisha madini ya plutonium.

Ilan ramon huyu alikuwa amepewa jukumu la kuandaa raman na kuangalia kama jets IAF zingeweza kwenda na kurudi salama. Ivry huyu aliamini kuwa Jets zingeweza kwenda kirahis na kulipua maeneo lengwa ila shida ilikuwa kurudi salama. Kutokana na umbali na teknolojia ya miaka hiyo ilikuwa ni shida kwenda na kurudi kwa umbali huo pasipo kujaza mafuta.

C:\Users\HAPPYD~1\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image001.jpg


Hii ni ndege ya Israel F-16A Netz 243 ambayo ailiendeshwa na Kanal Ilan Ramon katika operation Opera kwenda kulipua vinu vya nyuklia vya saddam huko Osirak mwaka 1981.

Arye Naor anasema kuwa waziri Mkuu alikuwa amedhamiria kulipua vinu hivyo kwa hali yoyote hata kama kwa kitendo hicho ndo ingekuwa mwisho wa uwaziri wake mkuu.

Upembuzi ukafanyika kuwa inawezekana jet moja au mbili zisiweze kurudi. Hivyo katika kujiandaa na shambulio hilo pilots wakaelekezwa kuwa wamejiandaa ikitokea wakashindwa kurudi au wakakwama huko basi watumie pesa za Iraq ambazo walikabidhiwa ili waweze kutoroka.

Baada ya kuwa mara ya kwanza waliahirisha operation hiyo wakaamua kuwa safari hii iwe Jumapili kwa sababu wataalamu wa Nyuklia wa Kutoka UFaransa watakuwa mapumziko. Na wakaambiwa kuwa waepuke mapigano ya uso kwa uso(dog fight) na ndege za Iraq ambazo walikuwa wamenunua Usoviet MiG ikiwa kulikuwa na ndege ya abiria maeneo karibu ili wasilipue ndege hizo na kusababisha vifo kwa wataalamu wa mataifa mengine hivyo kuibua mzozo. Kumbuka hapa kulikuwa pia kuna mambo ya kidiplomasia.

Hivyo ikapangwa safari ambayo haitakuwa mbali sana na zinapopita ndege za abiria za Iraq. Ndege za kijeshi za Israel ziliingia Iraq pasipo kutambuliwa na majeshi ya anga ya Iraq. Wakapiga vituo hivyo na kuviharibu kabisa. Iraq walipokuja kugutuka walikuwa wameshachelewa ilikuwa ni kama kufumba na kufumbua vituo vile vimelipuliwa na ndege za Israel ambazo mwanajeshi mmoja wa Iraq alisema zilikuwa ni Ghost(kitu kilichosababisha auawe na utawala wa saddam maana alionekana kuwa ame appreciate utaalam uliotumika kuja kuwashambulia nchini mwao)

Moshe Melnick ambaye alikuwa akiongoza Mawasiliano muda huo na mapailoti waliokuwa wakiendesha jets za mashambulizi aliwaambia kuwa mara wamalizapo tukio wakiwa wanarudi ndipo waweze kuwasiliana na makao makuu kutoa taarifa kuwa wapo salama salimini.israel hawakutaka kupoteza ndege wala mtu mmoja katika tukio hilo.

Anasema anakumbuka alikuwa Ilan Ramon ambaye alichelewea kutoa taarifa alipopiga na kukawa na kimya kirefu sana. Wote wakapatwa na mashaka lakini katikati ya mashaka hayo alisikika Ramon akisema kwa sauti ya utulivu kuwa he is safe and sound.salama salimini.

Kitendo kile cha kulipua vile vinu kililaaniwa na mtaifa mengi duniani ufaransa wakikasirika sana sababu walitumia pesa nyingi sana ktika ule ujenzi. Lakini Ivry anakumbuka mwaka 1991 aliyekuwa secretary wa USA Dick Cheney alimpa picha ya black and white kutoka angani ikionesha majengo yaliyoharibiwa na akisema kuwa “ mlirahisisha sana kazi yetu”

Akiwa anatoa tamko waziri mkuu akaanza kwa kusema kuwa operation ya kulipua vinu vya kinyuklia vya Iraq imefanikiwa sana . na uamuzi wa kulipua ulichukua miezi mingi iliyopita ukiwa na vikwazo vingi tulifikiria kwa kina na kuamua kuwa mwishoni hatukuwa na uchaguzi mwingine kwa sababu kama tungeshindwa kuamua kutenda sasa basi baadaye ingekuwa tumechelewa sana.

Israel wakaendelea kwa miaka mingi kutangulia mbele ya maadui yao na kufanya kuwa moja ya taifa lenye kuzungukwa na maadui wengi na lenye kuwa na intelejensia ya hali ya juu duniani. Kila mwananchi wa Israel ufahamu kuwa ni wmanajeshi wa akiba kwa maana siku ikipigwa tu filimbi ajikusanye kujiandaa na vita yupo standby. Wakati huo huo mossad wametapakaa dunia nzima wakiwa katika sura tofaut tofaut kama waarabu,waafrika wazungu,wachina,wahindi,wajapan n.k

Daa, si mchezo.
 
operation entebe nadhan nimewah kuileta ngoja niitafute. humu ndani. Mossad ni wazuri sana kuliko hata CIA au KGB ni wazuri sana. kiukweli hata mimi huwapenda. na mambo yao huwa ya kimya kimya sana.

Mimi nawalubali sana Mossad kuliko CIA.

Mkuu ukipata muda tuletee simulizi za Operation Entebbe zilizofanywa na Mossad na Jeshi lao la Israel pale Entebbe, Uganda.

Moja kati ya Operation ya kiwango cha juu kuwahi kufanyika.
 
"Mossad" imetisha kwenye hili jukwaa.
 
kwa story za daily za kijajusi humu ambazo...kiasi kikubwa waandishi wanaielezea MOSSAD kama ndio taasisi ya kijasusi iliyo imara na yenye kufanikiwa sana ktk opp zake za kijasusi...
na hii ni kutokana kuzungukwa na kiasi kikubwa cha maadui wanaoipinga.....
kwa makala zipitazo ktk jukwaa la intell....basi mossad ndio baba wa ujasusi duniani pamoja na udogo wake kitaifa.....
na mataifa yote makubwa na madogo itakuwa wanalitambua hilo......
 
Back
Top Bottom