- Source #1
- View Source #1
Wakuu
Nimekutana hii taarifa inasema kuwa Amnesty yaunga mkono Maria Sarungi kufukuzwa Kenya kuna ukweli wa hizi taarifa au ni uzushi?
Nimekutana hii taarifa inasema kuwa Amnesty yaunga mkono Maria Sarungi kufukuzwa Kenya kuna ukweli wa hizi taarifa au ni uzushi?
- Tunachokijua
- Madai
Ipo taarifa inayoeleza kuwa shirika la haki za binadamu la Amnesty International limetoa taarifa kwa Umma kuunga mkono kufukuzwa kwa Maria Sarungi nchini Kenya.
Taarifa hiyo pia imewekwa kwenye grafiki inayoonekana kuwa ni ya chombo cha habari cha millard Ayo.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefanya ufuatiliaji na kubaini kuwa taarifa hiyo haina ukweli.
Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao hauoneshi kuwepo kwa kumbukumbu zozote zinazoonesha kuwa Maria Sarungi amefukuzwa nchini Kenya hivi karibuni, hata yeye kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwemo X hajawahi kueleza kama amekutana na kadhia hiyo kwa hivi karibuni.
Pia inayoonekana kuwa ni barua ama taarifa kwa umma kutoka kwa Amnesty International ni ya kugushi na haijatolewa na shirika hilo. Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram shirika hilo halijatoa taarifa yoyote yenye kufanana na hiyo kwa siku ya Septemba 17, 2025.
Aidha grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo ni ya kughushi pia na haijachapishwa na chanzo hicho cha habari.