Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Nausikiliza huu wimbo hapa ofisini na unanipa hamu ya kufanya kazi. Shukrani kwa mwimbaji kuyatendea haki maneno yaliyomo ndani ya wimbo huu. Kaimba vizuri sana. Shukrani pia kwa mtunzi wake-Father G. Huyu bwana katunga nyimbo nyingi sana zilizovuma. Ni wakati sasa kuwaenzi watunzi wa nyimbo badala ya waimbai pekee. Tunzo hazitoshi.
Katika wimbo kuna baadhi maneno matamu kama hivi;
Na ukigusa moyo wangu ni wewe
ulobeba nafsi yangu ni wewe
huna wewe bila mimi, A'more
ulimwengu wote wajue ya kwamba ni wewe
A'more x5
usiumwe usiugue, uwe mzima daima
usisikize ya watu penzi letu kulitupa
na usibadili kipimo cha mapenzi unayonipa
sitokutoza ushuru, nitawale mi ni wako
pesa nyumba nayo gari si mali kitu kwangu
hata niwe jangwani wewe ni maji kwangu
una mapenzi ya kweli yao wote ya bandia....
sasa katika hili pamoja na maneno mazuri kwenye wimbo, ageutunga mwanamke ningefarijika zaidi. hii ni hali ya mwanaume anayeusemea moyo wa mwanamke. kwamba mwanaume anataka mwenza wake awe vipi.
ewe mwanamke;
ni kweli hutonitoza ushuru?
ni kweli pesa nyumba, magari si mali kitu kwako?
ni kweli mapenzi ya wengine ni ya bandia?
ni kweli nimebeba nafsi yako?
ni kweli ulimwengu wote wanatambua ni mimi pekee?
i wish ingekuwa hivi