GE2025 Amos Makala: Hakuna ambaye ameenguliwa au kukatwa kama ambavyo inaripotiwa kwenye Vyombo vya habari

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Naomba nisisitize, kwa utaratibu wetu wa Chama Cha Mapinduzi CCM mpaka sasa hakuna mtu ambaye ameenguliwa au kukatwa kama ambavyo inaripotiwa kwenye Vyombo vya habari. Nimeona wameandika huyu kapenya au huyu kafyekwa, huyu hayupo tatu bora- Kama nilivyosema mchakato huu wa uteuzi utahitimishwa na kikao cha Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi na hapo ndiyo itakuwa mwisho wa kupata majibu ya mchakato mzima wa Wagombea wanaoteuliwa kwenda katika kura za maoni

Kamati kuu itakapohitimisha tutatoka kuwaambia walioteuliwa kwenda katika kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi. Zamani nyie mnajua ilikuwa watu wote wakigombea wanakwenda kupigiwa kura za maoni kwahiyo tumesema utaratibu wa sasa watateuliwa wachache ili kwenda kupigiwa kura za maoni."- Amos Makalla, Katibu wa Itikadi na uenezi na mafunzo wa CCM akizungumza na waandishi wa habari Ofisi za Makao Makuu ya CCM Dodoma leo Jumapili Julai 13, 2025





Your browser is not able to display this video.
 
Anajijambia jambia tu anabishana na mfumo walioweka wao wenyewe.

Majina yatatoka kamati za wilaya kwenda kamati za mikoa kupata baraka, kuongeza au kupunguza halafu mwisho cc Taifa. sasa yeye anabisha nini ?? hopeless kabisa

Au anataka kusema waliofyekwa wengi watarudishwa na kamati ya Taifa, hata kama ni ndio sasa watarudishwa wangapi ?

Makalla hajui asemalo apuuzwe...
 
Taarifa inayosambaa mitandaoni kwa sasa ni kwamba hakuna mgombea au tuseme mtia nia kupitia CCM aliyekatwa

Chawa msipanic

Ayo tv 📺
 
Ni watu Gani hao wanaambiwa wasipanic n wagombea au wananchii 😁
 
WAmeona upepo unawakataa watajirudi hawa watu ni wapuuzi saana
 
Believing words of a politician is as stupid as believing a stripper loves you.​
 
SAWA BWANA MAKALLA , MUDA NI MWALIMU MZURI. WE WILL COUNTER-CHECK IF THE ONES NAMED TODAY ARE THE SAME AS THOSE OFFICIALLY RELEASED WHEN THE TIME IS RIPE
 
Taarifa inayosambaa mitandaoni kwa sasa ni kwamba hakuna mgombea au tuseme mtia nia kupitia CCM aliyekatwa

Chawa msipanic

Ayo tv 📺
Hoja ni kwamba nafasi ni moja inayotakiwa, wengine lazima watolewe,,sasa wanatolewa hata kama ni kwa vigezo halali,wataitwaje??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…