JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Akihojiwa na Clouds FM, Makalla amesema “Hilo jambo halipo, halijafika Halmashauri Kuu, CCM inaendeshwa na vikao, kikao cha Kamati Maalum Zanzibar halijafika.”
Awali, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa alinukuliwa akisema CCM Zanzibar imeona Serikali kuingia katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ni hasara na matumizi mabaya ya Fedha ndio maana wameona wawasilishe pendekezo la kuongeza muda wa kukaa madarakani."
Pia soma Kuelekea 2025 - CCM Zanzibar wapendekeza Rais Mwinyi atawale kwa miaka 7, wasema kufanya uchaguzi 2025 ni hasara na matumizi mabaya ya fedha za umma