Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Amos Makalla amewataka Wananchi wanaopeleka kero kwa Viongozi wa CCM wanaoendelea na ziara kwenye Mikoa mbalimbali, kupeleka kero za ukweli badala ya fitina huku akisema hatoshughulika na kero hizo hadharani kwakuwa nyingine ni za faragha.
Akiongea akiwa Mkoani Rukwa anakoendelea na ziara pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi, Makalla amesema “Kama kuna Mtu ana kero aje hapa mkutano utaendelea Mimi nitakusikiliza lakini kero iwe ya kweli isiwe fitina, na Mimi siwezi kufika nikatangaza hapa aah , kuna Mama jambo moja kanieleza jana faragha la ndoa sasa ningempandisha hapa aseme Mimi na Mume wangu tunagombana, aah nilikaa nae akanieleza nikampa Wanasheria wakamshauri”
“Kwa Watendaji wa Serikali Mkuu wa Mkoa na Ma-DC wana utaratibu wa kusikiliza kero, Wananchi nendeni kwenye kero msisubiri Viongozi wa Kitaifa lakini pia Watendaji mkiwasikiliza hizi kero za Wananchi hakikisheni mnatoa majawabu “
Pia soma
- Amos Makalla Mwenezi mpya CCM Taifa, Ally Hapi Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi