LGE2024 Amos Makalla: Mawakala wetu watalinda kura ipasavyo

LGE2024 Amos Makalla: Mawakala wetu watalinda kura ipasavyo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo, CPA Amos Makalla, amesema kampeni za chama hicho zilizofanyika kwa siku sita katika majimbo nane ya mkoa wa Dar es Salaam zimeonesha dalili za ushindi mkubwa kwa CCM.

Akizungumza kwenye mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika Mikumi, Morogoro, CPA Makalla amebainisha kuwa mikutano yote ya kampeni imeonesha mwitikio mkubwa wa wananchi, hali inayowapa uhakika wa ushindi.

Kupata matukio yote kwenye uchaguzi ingia hapa: LIVE - LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

“Kwa taarifa tulizonazo na mikutano ilivyokuwa ikiendelea, ni wazi kwamba CCM itashinda kwa kishindo. Nimefanya kampeni kwa siku sita bila kupumzika, na matokeo tunayotarajia ni ya kuridhisha,” amesema CPA Makalla.

Akizungumzia maandalizi ya siku ya kupiga kura, CPA Makalla amewataka wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla kuungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kushiriki zoezi hilo muhimu. Amesema Rais Samia ataongoza Watanzania kwa mfano mzuri kwa kupiga kura katika kituo chake Chamwino, Dodoma, kama alivyoanza kushiriki tangu hatua za kujiandikisha.

“Kesho (Jumatano) ni siku ya kupumzika kama ilivyotangazwa na Rais, hivyo nawaomba tujitokeze asubuhi mapema kupiga kura. Baada ya kupiga kura, turudi nyumbani kupumzika kwa sababu CCM inaamini kuwa mawakala wetu walioteuliwa watalinda kura zetu ipasavyo. Hakuna haja ya kubaki vituoni kwani mawakala wapo tayari kuwakilisha chama chetu,” amesisitiza CPA Makalla.

Aidha, Makalla amewahimiza wanachama wa CCM kuepuka vitendo vya vurugu au usumbufu wakati wa uchaguzi. “Tusifuate tabia za wale wanaochochea ukorofi kwa kubaki vituoni baada ya kupiga kura. Hili ni jambo lisilohitajika, kwani CCM tunaamini katika utaratibu na nidhamu,” ameongeza.

PIA SOMA
- LGE2024 - Kwa kauli hii ya Amos Makalla ya "Mwana CCM ukishapiga kura, rudi nyumbani", Upinzani jiandaeni kwa virungu vya polisi
 
Back
Top Bottom