Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Haya jamani mliokuwa na kiherehere kuhusu uchaguzi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM, mna salamu zenu huku kutoka kwa Makalla
Kaeni kwa kutulia
=======================================================
Chama cha Mapinduzi CCM kimewataka wanachama wake kuachana na watu wanaobashiri kuhusu mrithi wa nafasi ya aliyekuwa Makumu Mwenyekiti wa chama hicho Abdulahman Kinana kwani nafasi hiyo haigombewi ila inapendekezwa.
Hayo yamesemwa Leo Januari 7 ,2025 makao makuu ya Chama hicho Jijini Dodoma na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa,Itikadi uenezi na mafunzo CPA Amos Makalla wakati akizungumza na Waandishi wa Habari
CPA Makalla amesema nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti haigombewi Wala haijazwi fomu hivyo hakuna mchakato wowote wa mrithi wa nafasi hiyo badala yake atapatikana baada ya mapendekezo ya jina katika kikao cha Kamati kuu na Halmashauri kuu Taifa.
" Wale waliokuwa wakibashiri mrithi wa Kinana muda huo haupo badala yake mrithi tutampata kwa jina kupendekezwa kwenye vikao na tayari maandailizi yote yanaendelea kufanyika kupitia Katibu mkuu wa Chama chetu Dkt. Emmanuel Nchimbi, " Amesema CPA Amos Makalla.
Hata hivyo Katibu Mwenezi huyo ametoa taarifa wa uwepo wa Mkutano Mkuu CCM ambao utafanyika January 18 hadi 19 2025 Jijini Dodoma