Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amesema Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na mambo aliyoyafanya kwa Taifa anaingia katika rekodi ya Marais bora Afrika.
"Mimi nimewahi kuwa Bungeni, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uongozi wake ndio Rais anayeingia katika rekodi ya kupeleka pesa nyingi za maendeleo kuliko wakati wowote", amesema Makalla
Akizungumza na wanachama wa CCM mkoani Simiyu, Makalla ameongeza kuwa chini ya uongozi wa Rais Samia, Tanzania imebaki kuwa kisiwa cha amani, hali inayowawezesha wananchi kufanya shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo.