Amos Makalla, tekeleza matamko yako mkoa wa Dar es Salaam

Amos Makalla, tekeleza matamko yako mkoa wa Dar es Salaam

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,503
Reaction score
13,463
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Amos Makala umetoa matamko sana tangia ule kiapo cha kuwa Mkuu wa Mkoa, cha ajabu hakuna linalotekelezwa hata moja

1) Ulianza na machinga ukachimba biti weeeh mwisho siku hakuna lililotekelezwa.

2) Ukaenda kukagua mradi wa mwendo kasi Mbagala ukachimba biti ukatoa siku 3 wananchi watoke kupisha ujenze ila wananchi wamekugomea huko Mbagala.

3) Umetoa tamko la kuvaa barakoa na kukaa level seat kwenye vyombo vya usafiri lakini hakuna lililotekelezwa.

Mkuu wa Mkoa Amos Makalla unafeli wapi? Jitathimini kwanza kabla ya kutoa matamko ama sivyo itaonekana Hayati alikupiga benchi sio kwa bahati mbaya.
 
Kumrahishia kazi atoe Rai kwa trafiki kukamata daladala ambayo watu hawajavaa barakoa, watachangamkia sana
Jana kakaa na kikao na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa nafikiri mpaka Trifick wanahusika hapo lakini pia hali hii tofauti na kipindi covid inaanza ambapo Mkuu wa mkoa wakati uo Paul Makonda alitoa tamko nakumbuka ilikuwa jumamos kuwa kuanzia J3 kama huna barakoa marufuku kuingia mjin! Watu tulitafuta barakao wenyewe kwanza tulikuwa na hofu na ule ugonjwa lakini sasahivi wengi hawana hofu na Covid kwakweli.
 
Wenyewe mnasema hamtishiki na kakorona,tumafua tu,halafu mnataka awavishe barakoa kwa bakora,bakini na kutokuelewa kwenu,siku akili zikiwajaa hamtahitaji hata kukumbushwa kuvaa hiyo barakoa.
 
Jamaa ni debe tupu kabisa. Haiwezi Dar kabisa huyu. Watu tushamshitukia.
 
tumerudi kwenye matamko!
kiongozi anaamka hata hajapiga mswaki anaitisha waandishi wa habari na kuutangazia umma wa daslam

asante wanadaslam kwa kumgomea huyo wa kuja asiyeujua hata mitaa na kona za jiji hili

daladala tunapanda bila barakoa na hamtufanyi kitu
 
"Kajeba, post: 39828603, member: 61

asante wanadaslam kwa kumgomea huyo wa kuja asiyeujua hata mitaa na kona za jiji hili
Mkuu Makala si wakuja nimzaliwa wa hapahapa town. Wakuja ndiyo wanatuendeshaga kuanzia Makamba sr, Tibaigana na Makonda.
 
Huu mkoa wamrudishe tu Bashite maana alikua na amsha amsha sana.Ww angalia hata swala la usafi kila mwisho wa mwezi watu siku hizi wala hawalizingatiii.
 
Huyu bwana ameshatoa maagizo kama mara tatu hivi kwamba daladala katika jiji lake la Dar hazipaswi kusimamisha abiria na kila mtu lazima awe na barakoa.
Lakini hakuna chochote, abiria wanasongamana kama kawaida wala hakuna anejali barakoa.

Kuna kipindi MAKONDA alikuwa akitoa agizo kila kona ya jiji linatekelezwa na ukiliza watu vipi wanakwambia mkuu wa mkoa kasema!

Leo hii Makala anatoa agizo alafu kinaishia hewani tu tena hata ilala bungoni halivuki!

Point yangu ni kwamba nini kinafanya huyu bwana maaguzo yake kupuuzwa namna hii hata na askari?

My take:
Wakati nasona shule ya msingi, kuna mwalimu huyo alikuwa akishika zamu katika wiki yake, ikifika saa 12 asubuhi wanafunzi wote wako mstarini wameshika namba.
Na kuna mwalimu mwingine ilikuwa akishika zamu madogo hadi saa 4 bado wanawasili shuleni[emoji23][emoji23][emoji23].
 
Wakazi wa Dar es salaam ni manunda sana!

Sasa Jokate anaweza kuwapiga mkwara kweli!!!
 
Back
Top Bottom