Huyu bwana ameshatoa maagizo kama mara tatu hivi kwamba daladala katika jiji lake la Dar hazipaswi kusimamisha abiria na kila mtu lazima awe na barakoa.
Lakini hakuna chochote, abiria wanasongamana kama kawaida wala hakuna anejali barakoa.
Kuna kipindi MAKONDA alikuwa akitoa agizo kila kona ya jiji linatekelezwa na ukiliza watu vipi wanakwambia mkuu wa mkoa kasema!
Leo hii Makala anatoa agizo alafu kinaishia hewani tu tena hata ilala bungoni halivuki!
Point yangu ni kwamba nini kinafanya huyu bwana maaguzo yake kupuuzwa namna hii hata na askari?
My take:
Wakati nasona shule ya msingi, kuna mwalimu huyo alikuwa akishika zamu katika wiki yake, ikifika saa 12 asubuhi wanafunzi wote wako mstarini wameshika namba.
Na kuna mwalimu mwingine ilikuwa akishika zamu madogo hadi saa 4 bado wanawasili shuleni[emoji23][emoji23][emoji23].