Pre GE2025 Amos Makalla: WanaCCM watakaokatwa licha ya kushinda kura za maoni wakae kimya, wakati wao utafika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla, amewataka wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kuwa na subira.

Amesema watakaokatwa licha ya kushinda kura za maoni, wasiseme neno, badala yake wawe na uvumilivu kwa kuwa muda wao utafika, huku akiwatakia heri waliohamia vyama vingine, akidai kuwa ni suala la muda tu.

Aliwapongeza baadhi ya wagombea ambao majina yao yalikatwa na wanaendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za chama hicho, akijitolea mfano yeye mwenyewe kwamba kuna kipindi aligombea na kushinda kwa kishindo lakini jina lake halikurudi.

"Tunawatakia kila la heri waliokosa uvumilivu, wako ambao hata uteuzi haujafanyika wakahamia mtaa wa pili siku ya tatu wakageuza tena CCM, niwape salamu hao waliowaokoteza tumewaazima tu wagombea, watarudi Chama Cha Mapinduzi.

"Kuna wengine hata vikao hatujakaa niliona wanakaribishwa siku mbili jamaa akarudisha kadi akarudi CCM, hivyo niwaombe kuweni watulivu, tuna uchaguzi mwakani," alisema Makalla.

Chanzo: Nipashe
 
Then nini maana ya kura ya maoni kama wanashinda halaf wanakatwa? Kuna umuhimu gani wa hiyo kura?
 
Kwani maoni lazima yachukuliwe??
CCM inayo maamuzi bila woga na bila shaka na hiki ndio kinaifanya iendelee kuishi.
 
Siku Hizi Vyama vya Siasa vimechukua nafasi Ya Nasma wa Muungano na Hadija Kopa wa TOT 😂😂

Kwako mrangi Ova
 
Kwani maoni lazima yachukuliwe??
CCM inayo maamuzi bila woga na bila shaka na hiki ndio kinaifanya iendelee kuishi.
Basi futeni chaguzi za ndani hazina maana , kama chama tayari kina list ya watu inao wataka ya nini kupotezeana muda?
 
Nimeona insta page ya makala, jamaa anakula zoezi, yaani ukizikunja unapigwa, ukija jukwaani unapigwa
 
KATIBU wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla, amewataka wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kuwa na subira.

Amesema watakaokatwa licha ya kushinda kura za maoni, wasiseme neno, badala yake wawe na uvumilivu kwa kuwa muda wao utafika, huku akiwatakia heri waliohamia vyama vingine, akidai kuwa ni suala la muda tu.

Aliwapongeza baadhi ya wagombea ambao majina yao yalikatwa na wanaendelea kushiriki katika shughuli mbalimbali za chama hicho, akijitolea mfano yeye mwenyewe kwamba kuna kipindi aligombea na kushinda kwa kishindo lakini jina lake halikurudi.

"Tunawatakia kila la heri waliokosa uvumilivu, wako ambao hata uteuzi haujafanyika wakahamia mtaa wa pili siku ya tatu wakageuza tena CCM, niwape salamu hao waliowaokoteza tumewaazima tu wagombea, watarudi Chama Cha Mapinduzi.

"Kuna wengine hata vikao hatujakaa niliona wanakaribishwa siku mbili jamaa akarudisha kadi akarudi CCM, hivyo niwaombe kuweni watulivu, tuna uchaguzi mwakani," alisema Makalla.

Chanzo: Nipashe
Kama wana sifa na wamekatwa kimizengwe waende wakagombee kupitia vyama vingine. Hakuna kukaa kimya kama wahusika hawafuati utaratibu wa kidemokrasia.
 
Back
Top Bottom