TANZIA Amos Nnko, Mkurugenzi ofisi ya Msajili wa Hazina, bintiye wafariki ajalini Same

TANZIA Amos Nnko, Mkurugenzi ofisi ya Msajili wa Hazina, bintiye wafariki ajalini Same

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Nnko.jpg
Ajali zinazotokea msimu wa sikukuu zimeendelea kuacha majonzi kwa Watanzania, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ofisi ya Msajili wa Hazina, Amos Nnko kufariki dunia.
IMG-20241223-WA0017.jpg
Nnko amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Same, mkoani Kilimanjaro, jana mchana Jumapili, Desemba 22, 2024. Katika ajali hiyo, pia binti yake wa kwanza, Maureen Nnko amefariki.

Hayo yamethibitishwa na Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu leo Jumatatu Desemba 23, 2024 kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Katika taarifa hiyo, imeelezwa kuwa mke wa marehemu, Agnes Nnko na watoto-- Marilyn, Melvin na pamoja na mwanafamilia mwingine, Sylvana wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya KCMC na Mawenzi.



“Mipango ya mazishi inaendelea kuratibiwa na familia ya marehemu kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina,” imeeleza taarifa hiyo.

IMG-20241223-WA0001.jpg
 
Ajali zinazotokea msimu wa sikukuu zimeendelea kuacha majonzi kwa Watanzania, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ofisi ya Msajili wa Hazina, Amos Nnko kufariki dunia...
Aisee, kifo hakina substitution...we carry life and death.

Wapumzike kwa amani sisi sote ni wasafiri..
 
Kama ni mtu wa majukumu sana usiendeshe gari. Majukumu yanaleta uchovu wa akili na kuhamisha mawazo.
Tafuta vijana hapo mjini wakupeleke, halafu unawatoa na laki moja mbili
Bosi hakuna cha vijana tena vijana ndiyo ukute siku hiyo hajalala anausingizi au kachanganywa na demu au mke. Cha muhimu ni kuendesha kwa tahadhari tu na kuhakikisha gari imefanyiwa service kwa kila kitu. Kuna jamaa yetu alikufa tena akiwa na huyo unayemuita kijana. Kilichotokea yeye alikuwa busy so akawa akijisikia kachoka anamtumia kijana ila siku ya ajali kijana hakufa na yeye bosi akafa. So hakuna unafuu
 
Back
Top Bottom