Amphibious Vehicles

Amphibious Vehicles

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
5,489
Reaction score
14,091
Amphibious Vehicles ni magari yaliyotengenezwa Kwa ajili ya kutembea nchi kavu na majini.Magari haya yalikuwa yakitengenezwa kabla ya vita kuu ya pili ya dunia, mengi yalitumika katika jeshi.

UFANYAJI KAZI WA HIZI GARI
Hizi gari hutumia mfumo wa injini za magari za kawaida kwa ajili ya kuliendesha gari na gari inapo ingia katika maji hapa itatumia mfumo wa jet au propela ndogo zilizowekwa nyuma ya gari.

Gari hizi huweza kuingia popote kwenye maji bila ya kutegemea uwepo wa gati la kupaki boti au meli.Punde gari linapo ingia kwenye maji dereva hurusu mfumo wa jet au propela zianze kuzunguka ili gari lisogee majini.

images.jpeg


Kampuni mbalimbali za magari zimekuwa zikitengeneza Amphibious car, mfano Land Cruiser wana Amphicruiser,Jeep wana Jeep Panther,Man Diesel, Mercedes Benz na Land Rover.

JEEP PANTHER
Hii ni moja ya Amphibious car iliyojizolea umaarufu sehemu nyingi duniani kutokana na uwezo wake na spidi iwapo majini.

Ina injini yenye 305hp na inaweza kukimbia mpaka speed 128km/h iwapo barabarani na kwenye maji ina speed ya 72km/h (45mph au 45knots). Speed ya kwenye maji ndio imeleta heshima Kwa gari hii na kuzua mjadala wa hii ni gari au speed boat. Hii gari imefanya vizuri Sana kwenye mauzo.

Kwenye kuingia majini inatumia mfumo wa hydrolic ambao uzificha tairi ndani baada ya kubonyeza batani na kitendo cha kuficha tairi ndani kinachukua sekunde 15. Pia unaweza ukaingia kwenye maji na Kasi ya speed 24km/h bila kupata tatizo lolote.

Ubunifu ni kuwa imetengenezwa Kwa chasisi ya chuma na body yote imeundwa Kwa fiber glass na kuipa uwezo mkubwa wa spidi iwapo majini, hata kwenye jangwa na njia korofi hivyo kuwa na uwiano mzuri wa uzito.

download.jpeg

Hii gari Jeep Panther Kwa Afrika mashariki kuna wazungu waliwahi kuja nayo Kenya miaka ya 2016, wakati wakifanya matanuzi ufukweni na kukatisha maeneo ya bahari ya Hindi ilikuja kupelekea mzozo kwenye vyombo vya habari na mamlaka ya usimamizi wa vyombo vya majini Kenya wakabaki na mshangao kuhusu Sheria itayotumika Kwa gari kama hii.


Hao wazungu baadae wakaja na hii gari Tanzania, baadhi waliishuhudia ikipita maeneo ya Slip way,Coco Beach,Dar Yatch Club na maeneo ya fukwe za bahari ya Hindi.
 
Back
Top Bottom