Amri Said Kocha Polisi Moro:Kipigo cha Yanga kimeniogopesha,Nimeacha kazi!

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
Siku chache tangu aliyekuwa kocha wa muda wa Polisi Morogoro, Amri Said atangaze kubwaga manyanga kuifundisha timu hiyo, imebainika kuwa Yanga ndiyo chanzo.


Amri anadaiwa kufanya hivyo kutokana na kuhofia kipigo kutoka kwa Yanga kama ilichokumbana nacho Coastal Union ya Tanga cha mabao 8-0, kwa kuwa Yanga inatarajiwa kucheza na Polisi Moro hivi karibuni.

Amri alisema kukosa ushirikiano klabuni hapo ni sababu kubwa ya kujiondoa huku ikizingatiwa kuwa timu hiyo ipo katika nafasi mbaya kwenye Ligi Kuu Bara.

“Kila nililokuwa nikiwaambia waliona ni jambo la kawaida wakati timu ipo kwenye nafasi mbaya, nikaona ni bora nijiondoe kuliko kuja kuharibu CV yangu na ukizingatia timu hiyo bado hajacheza na Yanga, yasije kunikuta kama yaliyomkuta ndugu yangu Julio (Jamhuri Kihwelo, kocha wa Coastal),” alisema Amri.
 

Attachments

  • amri+said.JPG
    39.7 KB · Views: 419
Pole zake Amri Said mchezaji wa zamani wa Simba. Amesoma majira na nyakati!
 
Stand Utd tutakomesha ubabe wa Yanga hadi sasa tunaongoza 1 Bila dhid ya JKT Ruvu
 
Usitukane mamba kabla hujavuka mto,
Yanga habari nyingine, usifananishe na timu ya mchangani (simba).

Tunakuja Taifa hamtaamini hata sijui mlitufungaje!! Ila Muhibu atakuwa na majibu
 
Ni kwa mujibu wa soccervista
 

Attachments

  • 1429285922858.jpg
    19.6 KB · Views: 231
Ingekuwa makocha wote wanaachia ngazi kwa kuhofia matokeo yanayofuata, basi Yanga ingekuwa inaingia uwanjani bila kocha kwenye mechi zake dhidi ya Simba
 
Kwani Amri Said naye kocha?? Huyu Julio wanasafiria nyota za wenzao
 
sipati pich hapo kesho yanga ikishinda si ndo itaogopeka mpaka basi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…