Huyu ni gwiji ambaye sidhani kama ana mpinzani nchini na pia Afrika Mashariki nzima. Kwa karibu sana ni kama Mzee Shaaban Robert. Tanzania hatujui kuenzi wataalam etu wa jadi, mara moja moja huwa wanamtumia tu wakitaka ulaji wa aina aina hapa na pale!
Najua kuwa katika miaka kumi ijayo atatokea mtu atakaye fanyia utafiti wa PhD ya kiswahili kuandika maandiko ya Amiri Sudi Andanenga "Sauti Ya Kiza" halafu siku mbili tatu unasikia ni mkuu wa BAKITA wakati kiswahili cha huyo mtu kipo hoi bin taabani! Kwani ndivyo walivyotumia maandiko ya Shaaban Robert kupata Udaktari wao wakati kiswahili hawakijui kabisa!
Sababu hizi ndiyo zimesababisha BAKITA isiwe na meno wala sauti, zaidi ya kukoroma kuroma hapa na pale utadhania mahututi anayehitaji maji!!!