Amri ya kukazia hukumu haikatiwi rufaa (execution order or ruling is not appealable)

Joined
Apr 26, 2022
Posts
83
Reaction score
128
AMRI YA KUKAZIA HUKUMU HAIKATIWI RUFAA: KALEBU KUBOJA MJINJA Vs SHADRACK DANIEL TEMBE, CIVIL APPEAL NO. 24 OF 2020.

Hii kesi imetafsiriwa na kuletwa kwako nami Zakaria Maseke, Advocate Candidate.

FACTS (STORI YA KESI):

Shadrack Daniel Tembe alimshtaki Kalebu Kuboja Mjinja kwenye Mahakama ya Wilaya Tarime (kesi ya madai namba 26 ya mwaka 2015).

Shadrack Daniel Tembe aliposhinda kesi akaomba kutekeleza hukumu na tuzo aliyoshinda kwenye. (Civil Application No. 22 of 2019).

Kwenye maombi yake ya kutekeleza hiyo hukumu na tuzo akaomba itekelezwe kwa njia ya kukamata na kuuza (attachment and sale) nyumba ya mshtakiwa iliyopo Buhemba, Tarime.

Mahakama ikamkubalia ombi lake (the application was granted). Mahakama ikateua dalali Mr. Alex Mgabo T/A Magabo Auction Mart kutekeleza amri ya Mahakama ya kuiuza nyumba ya mshtakiwa.

Mshtakiwa (Kalebu Kuboja Mjinja) hakuridhika, akakata rufaa kwenda Mahakama Kuu, Kanda ya Musoma, akidai kwamba Mahakama ya Wilaya Tarime ilijielekeza vibaya kwa kushindwa kupitia vizuri ushahidi uliopo (for failing to evaluate the evidence on record), kukamata mali ya wanandoa (attaching the matrimonial property) na kushindwa kumuarifu kuhusu haki yake ya kukata rufaa (and failing to inform him of the right to appeal against).

Kesi ilipofika Mahakama Kuu, kwanza Wadaawa wote wawili walijiwakilisha wenyewe (both parties appeared in person) hawakuwa na Mawakili.

Jaji akawauliza wadaawa (wenye kesi au parties), waieleze Mahakama kama hii rufaa ni sahihi (the competence of this appeal).

Kimsingi, walitakiwa waiambie Mahakama kama amri ya kukazia hukumu au amri ya kutekeleza tuzo ya Mahakama inaweza kukatiwa rufaa (whether an execution order is appealable)?

Aliyekata rufaa (mshtakiwa) akasema ndiyo, kwamba execution order is appealable (inaweza kukatiwa rufaa) kwa sababu, kukata rufaa ni haki ya msingi kwenye Katiba ya Tanzania, ya 1977.

Mjibu rufaa (respondent) yeye hakuwa na cha kusema. Ila akaiomba Mahakama iamue kulingana na sheria.

Baada ya kuwasikiliza, Jaji akaendelea sasa kutoa uamuzi.

Swali ni je, amri ya kutekeleza tuzo ya Mahakama (kukazia hukumu) inaweza kukatiwa rufaa? (the issue is whether an execution order or ruling is appealable)?

Mahakama ikasema ni kweli, haki ya kukata rufaa ipo kwenye Katiba. Lakini inatumika kwa kufata sheria na kwa kutegemeana na aina ya kesi iliyopelekea huo uamuzi. Mfano huwezi kukata rufaa kama sheria imetoa nafuu au njia nyingine mbadala tofauti na rufaa.

Maamuzi yanayoweza kukatiwa rufaa yameorodheshwa kwenye kifungu cha 74 na Order XL ya sheria ya Mwenendo wa kesi za madai (the orders subject to appeal are listed in section 74 and Order XL of the Civil Procedure Code, Cap. 33 / kwa kifupi hii sheria tunaiita CPC).

Mahakama ikasema, amri iliyotokana na maombi ya kutekeleza tuzo (kukazia hukumu) haipo kwenye hiyo orodha ya vifungu tajwa hapo juu. Kwa hiyo huwezi kukata rufaa. (An order arising from the execution proceedings is not listed in the said provisions. It is therefore not appealable).

Lakini, hiyo haina maana kwamba amri ya kukazia hukumu (execution order) haiwezi kupingwa Mahakamani (cannot be challenged).

Baadhi ya njia za kupinga amri ya kukazia hukumu kwa mtu aliyeghafirika ni kuomba mapitio (revision) ya kesi husika, au kufungua kesi ukishtaki kuhusu masuala yanayohusiana na utekelezaji wa tuzo (kukazia hukumu) chini ya kifungu cha 38 au kutumia Order XLI, Rule 1 ya
sheria ya mwenendo wa kesi za madai (CPC)

Kwamba, (the remedies available to a person aggrieved by the execution order or proceedings include, applying for revision of the execution proceedings, litigate the questions relating to execution under section 38 of the CPC or make use of Order XLI, Rule 1 of the CPC)

Lakini kwenye hii kesi, mshtakiwa aliipinga amri ya kukazia hukumu kwa kukata rufaa, kwa hiyo Mahakama ikasema rufaa sio sahihi. (the execution ruling/order for attachment and sale of the appellant's property to satisfy the decree has been challenged by way of appeal.)

The Court was of the view that “this appeal is incompetent.” Rufaa ikafutwa (struck out).

Hiyo ilikuwa tarehe 28/01/2021 katika Mahakama kuu ya Tanzania, Musoma.

------Mwisho-------

Natoa angalizo, wale wazee wa kukopi machapisho ya watu na kuweka majina yenu. Ni kosa kisheria. Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayejimilikisha andiko hili.

Unaruhusiwa kabisa kushare lakini usibadili yaliyomo. Ni heri uanze kuandika ya kwako mpya.

Tafsiri na stori hii ya kesi hii *meandaliwa na kuletwa kwako nami Zakaria Maseke. (0754575246 WhatsApp) zakariamaseke@gmail.com
 
Nilidhani ni Court of appeal, kumbe ni HC ambazo majaji wake walio wengi wamepewa kama zawadi not on merit and therefore maamuzi yao yanapinduliwa sana CA! All in all sante kwa andiko lako la weledi mkubwa!
 
Mkuu nakuelewa sana! Asante sana kwa elimu ya kisheria,usichoke lete vitu wasomaji tupo! Watoto wa Mujini wanasema tunakula utirio mwanawane!!!
 
Back
Top Bottom