Amshambulia mkewe kwa kuchinja Jogoo la Krismasi siku 10 kabla ya Sikukuu

Amshambulia mkewe kwa kuchinja Jogoo la Krismasi siku 10 kabla ya Sikukuu

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 50 kutoka wilaya ya Budaka mashariki mwa Uganda, amemjeruhi mke wake vibaya baada ya mwanamke huyo kumchinja kuku aliyetakiwa kufanywa kitoweo kwenye siku kuu ya Krismasi.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, bwana huyo alimnunua kuku kwa Sh.15,000 za Uganda (zaidi ya Tsh. 9000) akipanga kumchinja siku ya Krismasi, lakini kwa bahati mbaya mke wake aliamua kumchinja na kumuandaa siku ya Jumapili tarehe 15 Disemba.

Kwa mujibu wa katibu wa habari wa eneo hilo, Bw Joseph Gadimba, amesema baada ya mume kugundua kuwa kuku huyo hayupo tena, alimpiga mke wake na kumlaumu kwanini amemchinja bila ruhusa yake.

Bw Gadimba amesema ''alimpiga na kumchapa mke wake mara nyingi, huku akimuacha akipigania uhai wake.

Kwasasa mwanamke huyo anatibiwa katika kituo cha afya cha Budaka, mashariki mwa Uganda.

Wakazi wa eneo hilo walimtaka mwanaume huyo achukue majukuu yote yanayohusu matibabu ya mkewe ambayo alikubali kugharamia na kupelekea kesi hiyo kutoripotiwa polisi.

''Pale mwanamke huyo atakapo pona, ndugu zake kutoka eneo la Kapyani-Kasasira katika wilaya ya Kibuku, wanatarajia kufanya kikao na mwanaume huyo kujua chanzo cha yeye kumpiga mtoto wao na kutatua kesi hiyo,'' alisema Gadimba.
 
"Eti kikao cha kutaka kujua chanzo cha yeye kumpiga mke wake" sasa simehaambiwa kachinja jogoo
 
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 50 kutoka nchini Uganda, anaripotiwa kumshambulia Mke wake kwa kumpiga, baada ya kumchinja Jogoo wake aliyepanga aliwe siku ya Sikukuu ya Christmas.

Ripoti inasema mwanaume huyo alimnunua kuku huyo kwa pesa ya Uganda Shilingi 15,000, kisha kumpeleka kwa Mke wake na kutoa maagizo kwamba atachinjwa katika sikukuu hiyo.

Kwa mujibu wa Daily Monitor Mkewe huyo alikiuka maagizo na kumchinja siku ya Jumapili ya Disemba 15,2019, ndipo Mume wake alipatwa na hasira kisha kumpiga nusura ya kumuua.

Kwa mujibu wa afisa wa mawasiliano wa eneo hilo Joseph Gadimba amesema kuwa,

“Mwanaume alimpiga sana Mke wake nusura ya kutaka kumuua, Mwanamke huyo kwa sasa anapatiwa matibabu katika kituo cha Afya cha Budaka, kesi hii bado haijafika Polisi ila tumeamuru mwanaume huyo anatakiwa atimize majukumu ya kumgharamia hadi atakapopona” amesema Gadimba.

Aidha Gadimba ameongeza kuwa “Mwanamke atakapopata nafuu ndugu na wazazi wa pande zote mbili watafanya kikao ili kumaliza tofauti zao na kuwaunganisha tena wakae pamoja” .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huu ndio uanaume!
mwanamke lazima afuate na kutii maagizo toka kwa mumewe
 
thats good,
as a wife she has to reciprocate in turn what her husband say
 
hatari mbaya, unajua ugumu wa maisha utengeneza hasira/ukichaa.

sasa uwa inahitajika tu kisababishi moto uwake. hatare

Hasara Umfika Mwenye Mabezo
 
Back
Top Bottom