Amtwanga talaka mkewe

Huyu Mwenegoha ni laana tu inamtafuna. Najua anakoelekea ni kubaya zaidi.
Ushauri wa Bure amrudie Mungu wake!
 
Nyie KKKT mbona mnatukwaza siye waamini? Mara mkuu anunuliwe VX V8 na fisadi, mara mkewe apewe MarkX na mtoto wa fisadi, ni nini jamani? Ebu tafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na hayo yote mtarudishiwa.

Sasa KKKT inahusikana na nini hapa??? "Mnakwazwa" na KKKT au hao walionunuliwa VX V8? KKKT na mtu mmoja mmoja ni issue mbili tofauti - hata kama huyo mtu mmoja ni mkuu wa KKKT.
 
'marriage crisis' hakika wanajua kinachowagombanisha na nina hakika kati yao hakuna mwenye gatsi za kuweka sababu bayana!
kuna jambo halijaenda sawa 'kwa chumba'
mix with yours
 
Huyu Mwenegoha ni laana tu inamtafuna. Najua anakoelekea ni kubaya zaidi.
Ushauri wa Bure amrudie Mungu wake!

Ni kweli mkuu. Yampasa akae atafakari vizuri huo uamuzi wake. MUNGU hadhihakiwi. Maisha yake hayako mikononi mwake kujiamulia laana na baraka bali MUNGU ndo mwenye mamlaka hayo. Anapaswa alijue hilo ili atubu na kumrudia MUNGU.
 
Nyie KKKT mbona mnatukwaza siye waamini? Mara mkuu anunuliwe VX V8 na fisadi, mara mkewe apewe MarkX na mtoto wa fisadi, ni nini jamani? Ebu tafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na hayo yote mtarudishiwa.
matendo, jamani matendo, matendo kama kweli ninamcha Mungu mtanitambua tu.
 
.
Sio siri huyu Mwinigoha kama hali bangi kisiri basi ana pepo mkubwa sana wa ngono. Ona sababu anayoitoa ya kumtaliki mkewe haina nguvu ya aina yoyote kidila zaidi ya kuitukana imani ya kikristo. KKT mna kazi ya ziada.
mkuu

unaweza ukawa sihihi kwa upande wako, lakini naomba nikwambie kwamba tatizo la mwenegoha siyo ngono, tatizo lake kubwa ni kwamba haambiliki... ni mtu anayeamini kwamba yeye tu yuko sahihi

hata ajira yake pale KKKT iliota mbawa kwa sababu hiyo, yeye si mdini, yeye si mlevi na yeye si kwamba ana laana ya ngono... ila yeye ana kiburi cha kupitiliza na ni type ya either you are with me or you are my enemy
 

IT LOOKS LIKE UNAMFAHAMU VIZURI SANA HUYU BWANA , NA UNAJUA VIZURI HABARI ZA NDOA YAKE, KWA NINI USIWE WAZI KUIONGEA HUMU ILI NA SISI TUJUE UKWELI KULIKO KUHISI Tu?
 
Kila nyumba ina matatizo na yanazidiana.. Hakuwa na uvumilivu.. NDOA ni KUVUMILIANA.
 

Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni, haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, upendo hauoni uchungu, upendo hauesabu mabaya, upendo haufurahii udhalimu bali hufurahi pamoja na kweli, huvumilia yote, hutumaini yote, hustahimili yote, upendo haupungui neno wakati wote
 

.... Na zaidi ya yote Upendo ni zaidi ya tendo la ndoa!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…