Amunike Amuongeza Erasto Nyoni timu ya Taifa

Game ngapi huko manyau nyau stars walishapigwa ?
 
Nani kafunga hizo goal za stars ?
Amefunga Msuva na Samatta, Samatta pia amekosa penati iliyogonga mwamba wa juu.
Wachezaji wapya walioanza leo tofauti na mechi iliyopita ni Kapombe, Nyoni na Yondani wakichukua nafasi za Ulimwengu, Kessy na Mwantika.
Ulimwengu na Kessy walikuwa na kadi mbili za njano ila ukweli Ulimwengu ni mizinguo bora kocha amelazimika kuona wengine.

Mechi ijayo itakuwa dhidi ya Lesotho kwao na tutamkosa Samatta kwa sababu ana kadi mbili za njano. Na amini nimekupa mwanga kidogo wa kilichotokea.
 
Poa wamejitahidi next time wamfunge Lesotho pia
Kiukweli leo wamejitahidi ila bado tuna mapungufu beki hata umaliziaji sio mzuri mwalimu ayaangalie hayo.
Hivi mara ya mwisho Stars kushinda ugenini ilikua lini?.
 
Kiukweli leo wamejitahidi ila bado tuna mapungufu beki hata umaliziaji sio mzuri mwalimu ayaangalie hayo.
Hivi mara ya mwisho Stars kushinda ugenini ilikua lini?.
Labda tulipomfunga Chad nyumbani
 
Itakuwa mechi nzuri wakijitahidi watashinda..
Lesotho watakuwa relaxed wakijua samatta hayupo na watakuwa wako nyumbani hivyo watacheza kwa kushambulia stars wakijipanga watashinda
 
This time si zinaqualify team mbili kila group ?
Ndio zitaenda mbili, kimahesabu tunayo nafasi ila bado tuna mlima mkubwa wa kuupanda. Hawa Lesotho wanaweza kutuharibia mkuu.
 
Itakuwa mechi nzuri wakijitahidi watashinda..
Lesotho watakuwa relaxed wakijua samatta hayupo na watakuwa wako nyumbani hivyo watacheza kwa kushambulia stars wakijipanga watashinda
Kwanin samatta asiwepo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…