Amunike ni dhaifu kusoma mchezo na kubadilika

MTAZAMO

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
19,675
Reaction score
33,583
Wakuu,

Kocha wetu ni dhaifu mno kusoma mchezo na kubadili mbinu. Timu inacheza vile vile hata wapinzani wanapobadili mbinu. Mbaya zaidi kilema kikuu ni kocha kutojua namna ya kutumia viungo wetu. Hivi unamtumia kiungo kama Himid asaidie nini? Yule ni mkabaji tu na hawezi kuchezesha timu.

Badala ya kuingiza mtu wa kutuliza timu au kuongeza kasi ya mashambulizi unaingiza mkabaji tu na kufanya timu ielemewe. Nyoni aliomba sub mapema lakini haikufanyika hadi akalala chini na bado hawakufikiri haraka namna ya kujaza lile gap muhimu.

Amunike anafaa kuwa mkufunzi wa TFF kuendeleza program za soka lakini si mwalimu mzuri kabisa. Hakuna mechi aliyofanya sub za maana na akifanya ni too late damage inakuwa imeshakuwa kubwa na habadiliki haraka kwa kuwasoma wapinzani.

Wachezaji wanapambana wenyewe bila mbinu za ziada. Kwa timu hii hii angepatikana kocha anayewajua vizuri wachezaji wetu na anayeweza kubadilika kutokana na mchezo miujiza ingetokea.

Zambia walichukua hili kombe wakiwa hawana mastaa wa kutisha kulinganisha na wapinzani wao wengi. Technical bench ni msingi muhimu sana kabla hata ya timu yenyewe.

Wachezaji wetu wamepambana kwa uwezo wao wote lakini benchi la ufundi limewaangusha sana. Wasisingizie uzoefu mdogo, akina Okwi wana uzoefu gani? Jana tulihitaji uzoefu gani? Tatizo ni mbinu za kimichezo hatuna.
 
Huyu hata challenge cup hawezi kuchukua. Simba wamemuacha Kotei sababu za kucheza kama Himid. Kiungo mkabaji ambaye hawezi kuchezesha timu inafanya timu ilemewe tu. Bora angeingia Fei Toto angeongeza pressure kwenye kiungo.
Ndicho nilichoshangaa hivi Mao ana kipi cha ziada mpaka anapewa kipaumbele mle dah
 
Mnambebesha Amunike gunia la misumari sasa baada ya team CCM awamu ya tano kulamba flat
Amunike ana makosa yake toka zamani mnooo tulishamkataa na tunaendelea kumkataa...... Kingine hii team kuingizwa kwenye mkono wa siasa ni janga pia
 
Mnambebesha Amunike gunia la misumari sasa baada ya team CCM awamu ya tano kulamba flat
Wanakaa kusingizia hatuna experience! Hivi kama ni experience ukilinganisha wachezaji mmoja mmoja wa Senegal vs Algeria kutokana na ligi wanazocheza si mbingu na ardhi? Achilia mbali baadhi ya wakali wa Algeria? Lakini wameshinda kimbinu. Hata Uganda wanashinda kimbinu kuliko kutegemea skills za mtu mmoja mmoja.

Hivi unapomuingiza Himid unategemea matokeo gani? Wakati Nyoni anatoka akibebwa uliona walau kocha akielekeza quick cover up? Benchi la ufundi ni bovu tusitafute visingizio vya experience.
 
Kujenga umoja na upendo kwenye timu ni kitu muhimu sana, wachezaji wanatakiwa kucheza kwa amani.

Mawasiliano kati ya wachezaji uwanjani ni muhimu, wqchezaji wajue kusomana body language na kujua tukio linalotakiwa lifanyike na linalofuata baada ya hili.

Chakula kama Ndungai alivyosema, kukimbia dakika 90 si mchezo. Vijana wapigwe pa Protein, vegetables na wanga pia wapewe mazoezi mazito.

Baada ya dakika 45 za mwanzo unaona nguvu zilianza kuwaishia, hawakua na morari walioanzia.
 
Sasa benchi la ufundi lilipaswa kuanzia hapo. Hatuna wachezaji wenye uwezo wa kusoma mchezo na kubadilika. Timu kama yetu inabidi itegemee mbinu kutoka benchi la ufundi. Kipindi cha pili kilivyoanza akina ulimwengu walipaswa kutoka mapema na kuingiza watu wenye kasi ili kiungo na beki kisielemewe. Usisahau Kenya kiungo yupo Wanyama pia.

Mudathiri pia angebadilishana na Fei Toto au Domayo bado timu ingecheza kwa kunguvu bila kukaribisha mashambulizi mengi. Ila unatoa mchezeshaji kama Mudathiri inaingiza mkabaji tu kama Himid unategemea nini?
 
Wakuu,

Kocha wetu ni dhaifu mno kusoma mchezo na kubadili mbinu. Timu inacheza vile vile hata wapinzani wanapobadili mbinu. Mbaya zaidi kilema kikuu ni kocha kutojua namna ya kutumia viungo wetu. Hivi unamtumia kiungo kama Himid asaidie nini? Yule ni mkabaji tu na hawezi kuchezesha timu.

Badala ya kuingiza mtu wa kutuliza timu au kuongeza kasi ya mashambulizi unaingiza mkabaji tu na kufanya timu ielemewe. Nyoni aliomba sub mapema lakini haikufanyika hadi akalala chini na bado hawakufikiri haraka namna ya kujaza lile gap muhimu.

Amunike anafaa kuwa mkufunzi wa TFF kuendeleza program za soka lakini si mwalimu mzuri kabisa. Hakuna mechi aliyofanya sub za maana na akifanya ni too late damage inakuwa imeshakuwa kubwa na habadiliki haraka kwa kuwasoma wapinzani.

Wachezaji wanapambana wenyewe bila mbinu za ziada. Kwa timu hii hii angepatikana kocha anayewajua vizuri wachezaji wetu na anayeweza kubadilika kutokana na mchezo miujiza ingetokea.

Zambia walichukua hili kombe wakiwa hawana mastaa wa kutisha kulinganisha na wapinzani wao wengi. Technical bench ni msingi muhimu sana kabla hata ya timu yenyewe.

Wachezaji wetu wamepambana kwa uwezo wao wote lakini benchi la ufundi limewaangusha sana. Wasisingizie uzoefu mdogo, akina Okwi wana uzoefu gani? Jana tulihitaji uzoefu gani? Tatizo ni mbinu za kimichezo hatuna.
Mimi hata siiumii umeme uliisha kwetu usiku wa manane Kwan vip tiyri nn
 
Sikuona umuhimu wa Himid mechi ya jana, timu ilipaswa kushambulia zaidi maana wakenya walishaogopa, kocha akaanza kulinda tukapigwa
Manula mipira ya set pieces na kona bado ni tatizo kwake,
Kufungwa kunauma jamani, yaani tumbo lilijaa ghafla naenda chooni hamna kitu
 
Kocha wa Kenya alisoma game mapema na akafanya sub dakika ya 32 huku watu wakishangaa how come anafanya sub "mapema" hivyo. Baada ya hapo game ilichange kabisa. Kocha wetu yeye alikuwa amekunja mikono tu. Sijui ndio yalikuwa maagizo ya Prince DAB?
 
Amunike Ameunga Mkono Juhud za Mh Rais
 
Back
Top Bottom