Amuua mama yake akidai "ameishi kupita kiasi"

BRAVER

Senior Member
Joined
Jun 23, 2015
Posts
105
Reaction score
95


Wadau hiyo ni habari niliyoikuta kwenye gazeti moja la leo.
Tutafakari inakuwaje mtoto wa kuzaa wewe mwenyewe anakosa mapenzi na wewe mzazi wake?
Haya maoni yatiririke

Sent using Jamii Forums mobile app


====


MAHAKAMA ya Nanyuki Jumanne ilishuhudia kisa cha mwanamume kushtakiwa kumuua mamake mzazi akiwa na umri wa miaka 89 ambapo mshtakiwa alidai kuwa aliafikia ukatili huo kwa msingi kuwa mamake huyo alikuwa ameishi "kupita kiasi".

Satar ole Sanangi, 40 ambaye ni baba wa watoto wanne alifikishwa mbele ya hakimu Jesse Nyagah akidaiwa kumuua mamake, Kuyano Lesanangi mnamo
Julai 14.

Kiongozi wa mashtaka, Osman Mohammed alielezea mahakama vile mshtakiwa alifika nyumbani akiwa mlevi chakari na kisa akamvamia mamake mzazi akiwa katika boma lake.

“Mshtakiwa alifululiza hadi ndani ya nyumba ya mamake na akaanza kumzomea kuwa alikuwa hafai kuwa hai,” akasema kiongozi huyo wa mashtaka.

Ilibidi hakimu kwa wakati mmoja kuonya waliokuwa kortini dhidi ya kupiga usiahi dhidi ya mshtakiwa kwa sauti ya juu.

Aliongeza kuwa mshtakiwa alianza kuorodhesha majina ya waliokuwa rika la mamake lakini walikuwa tayari wameenda zao kuzimu.

“Mshtakiwa alimwelezea mamake kuwa hata yeye alikuwa anafaa kuondoka ulimwenguni ili aende waliokuwa wakongwe wa rika lake,” Mohammed
akaongeza.

Ndipo, korti ikafahamishwa, mshtakiwa alichukua fimbo na kumtandika mamake ili kumuua.

Mahakama ilifahamishwa kuwa kisa hicho kilitendeka katika kijiji cha Olesirikon Wilayani Laikipia Magharibi, hali ambayo ilimwacha mwathiriwa katika hali mbaya.

“Mwathiriwa alipelekwa hospitalini ambapo alitangazwa kuwa marehemu kutokana na majeraha aliyokuwa amepata katika kipigo hicho kutoka kwa mwanawe,” akasema kiongozi wa mashtaka.

Baada ya kukataa mashtaka ya mauaji na kuwa mlevi na kusabaratisha amani ya umma, Hakimu Nyagah alimwachilia mshtakiwa kwa dhamana ya Sh200,000 na mdhamini wa kiasi kama hicho.

Kesi yake itaanza kusikizwa rasmi Agosti 2, 2017.
 
Inasikitisha sana, lakini wakati mwingine hii inatokea endapo mtoto hakupata mapenzi mazuri kutoka kwa wazazi tangu akiwa mtoto mdogo. Kwa mfano mtoto alililewa katika mazingira ya shule za mbali na wazazi (boarding) tangu akiwa mtoto mdogo sana hadi amekuwa mkubwa hivyo basi hajapata ule upendo wa wazazi na haoni thamani ya wazazi zaidi ya kuwa karibu sana na marafiki kuliko ndugu na wazazi wake. Hilo ni fundisho kwetu namna ya kulea watoto wetu.

Love is all what we need!
 
Mama yake inawezekana ndio yule mhenga aliyesema, Kuishi Kwindi ndio kuona Mengi
 
"Siku za miaka yetu ni miaka sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini;..." ZABURI 90:10

sent from servant of God
 
@Satar amegeuka iziraeli mtoa roho kwa mama yake mwenyewe.
 
Inawezekana anavuta sigara kubwa "ingambo ingali"
 
Hii inaweza kuwa ni sababu ya msingi Kama kule Ulaya mtoto anapelekwa boarding school kuanzia chekechea mpaka anaanza maisha yake. Mzazi nae akizeeka mtoto anampeleka baba/mama yake old care centre -kambi ya wazee na kwenda kumsalimia tu weekend. Tanzania haya yameisha Anza. Mtoto anatamani likizo iishe arudi shule

Sent using Jamii Forums mobile app
 
So sad and not fear to kills your mom or another person.
We need to love each others don't care how we are.......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…