Amuua Mpenzi Wake Baada ya Kuambiwa Hayawezi Majambozi

Amuua Mpenzi Wake Baada ya Kuambiwa Hayawezi Majambozi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
4091218.jpg


Mwanaume mmoja nchini Uingereza amefikishwa mahakamani kwa kumuua mpenzi wake aliyemkebehi kuwa ana uume mdogo sana hivyo hawezi kumtosheleza hamu zake za kimapenzi. Peter Ling, 50, aliiambia mahakama kuwa alishindwa kuzitawala hasira zake baada ya kipenzi chake Linda Casey kumwambia kuwa hana kiungo cha siri kikubwa cha kuweza kumtosheleza hamu zake za kimapenzi, limeripoti gazeti la Daily Mail la Uingereza.

Ling, aliandaa sehemu ya starehe jijini London kwaajili ya kukutana na Linda akiwa na nia ya kumuuliza kama Linda ana mwanaume mwingine pembeni.

Baada ya kukutana na baadae kufanya naye mapenzi, Ling alimgeukia Linda na kuanza kumhoji kuhusiana na emails alizozituma zinazohusiana na tovuti za kutafuta wachumba na pia kama ana mwanaume mwingine pembeni.

Wakati wa mabishano yaliyozuka wakati huo, Linda aliongelea masuala ya viungo vya siri vya Ling akimuambia kuwa uume wake ni mdogo sana kuweza kumtosheleza.

"Nilikuwa ni kama bomu lililokuwa likisubiria kulipuka wakati wowote, alipotoa maoni hayo moja kwa moja yalizama kwenye akili zangu", Ling aliiambia mahakama.

"Siku zote nimekuwa nikiushuku ukubwa wa uume wangu", aliongeza Ling.

Baada ya Linda kutoa maoni hayo, Ling alianza kumshushia kipigo Linda mpaka alipofariki.

Ling anaitaka mahakama iamue kesi hiyo kama mauaji bila kukusudia badala ya kesi ya mauaji ya kukusudia aliyofunguliwa.

Kesi hiyo inaendelea.
 
Kamanda wangu punguza kasi ya kuweka posts! Inakuwa kero sasa!!
 
mwacheni atachemsha tu mwisho wa kuni ni mjivu
conquest
 
Mwacheni ustaadh utahabarishe bana. Nyie tatizo lenu ni nini?
 
Kamanda wangu punguza kasi ya kuweka posts! Inakuwa kero sasa!!
Wewe upo humu Tangu 2008 umechangia nini zaidi ya kupiga watu vita? umejiunga humu kazi yako kupinga watu wengine ngojeeni uchaguzi tuone kama kweli mnaweza kuwapinga viongozi wenu mukawachaguwa viongozi wengine ( MIAFRIKA BWANA NDIVYO ILIVYO)
 
Back
Top Bottom