Amuua mpenziwe baada ya kumfumania akinywa ARV kwa kificho

Msukuma wa dar

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2016
Posts
1,160
Reaction score
1,195
Mwanamke mmoja katika wilaya ya Hoima mashariki mwa Uganda anashikiliwa kwa madai ya kumuua mpenzi wake baada ya kumfuma akimeza dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARV)

Polisi wamesema siku ya Alhamisi kuwa Emmanuel Tumusiime, 35 alishambuliwa mpaka kuuawa katika makazi yake akiwa mji wa Kigorobya majira ya saa kumi na mbili jioni siku ya Jumatano.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor nchini Uganda, msemaji wa polisi wa mji huo, Bwana Julius Hakiza amesema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa Tumusiime alipigwa kichwani na shoka.

''Alipogundua kwamba mpenzi wake amefariki, mshukiwa alifunga nyumba na kupanda Bodaboda mpaka kwenye kituo kikuu cha polisi cha Hoima na kuripoti kesi ya mauaji,'' alieleza Bw. Hakiza.

Katika kituo hicho cha polisi, mwanamke huyo alikiri kumuua mpenzi wake.

Mwanamke huyo anadai kuwa alijisikia uchungu sana baada ya kuhisi kuwa kuna uwezekano ameambukizwa virusi vya Ukimwi.

Alikamatwa na kushikiliwa kwenye kituo kikubwa cha Hoima akishutumiwa kwa kujihusisha na mauaji.

Wapelelezi walikimbilia eneo la tukio na kulifunga kwa ajili ya uchunguzi zaidi, alieleza Hakiza.

''Tunatoa wito kwa waathirika wa virusi vya Ukimwi mara zote kuwapa taarifa wenza wao na kuhudhuria vituo vya ushauri nasaha na kufahamu kwamba kwa kuwa mwathirika, haimaanishi ni mwisho wa maisha,'' alishauri Hakiza

Nikiripotiiii kutoka Hoimaaa, Mimi ni Joniiiiiiiiiii Maratuuuuuuuuuuuu... BiiiiiibiiiiiiiiSiiiiiiiiiiii
 
Huu uzi ushindikizwe na hii picha kiukweli
IMG-20191213-WA0013.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee.Tunasoma humu kila siku habar za watu kutumia PEP/PrEP sijui pindi wanapohis wamepita mahali ambapo si salama hivyo kuhis wamaukwaa so wanajaribu kuwawahai virusi.

What if kama jamaa alikua anakunywa kwasababu hiyo?

Na kama ameathirika kwel na hataki kumshirikisha mwenzake,kwann alikua anakaa na hiz kitu ndani na kuzitumia humo humo badala ya mahala m badala ili asigundulike???

Sema , siku ikifika imefika tu
 
Back
Top Bottom