Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Msichana mwenye umri wa miaka 22 aitwaye Tiffany Gray ambaye ni Mshukiwa wa mauaji ya Sugar Daddy wake, Fasil Teklemariam (53), yupo rumande akishutumiwa kumuua Fasil na kisha kumkata kidole gumba ili kutumia programu yake ya benki na Uber.
Tukio hilo lilitokea April mwaka huu huko Washington DC ambapo Polisi wanaamini Tiffany Gray alimuua Fasil ndani ya nyumba yake kwa kumchoma kisu na kumuumiza kichwani kisha kumkata kidole gumba ambacho bado hakijapatikana.
Shahidi amewaambia Wachunguzi kwamba Gray na Washirika wake walitumia kidole gumba kwenda kutoa pesa kisha wakanunua bangi na pombe.
Picha za uchunguzi kuzunguka jengo la ghorofa la Teklemariam katika sehemu ya Manor Park ya DC zimeonesha Gray na Mwanamke mwingine, Audrey Miller, 19, pamoja na Wanaume wengine wawili, wakiingia na kutoka katika jengo hilo wakati wa mauaji hayo.
Teklemariam alikutwa amefariki katika chumba chake cha kulala Aprili 5 akiwa amezungukwa na glasi iliyovunjika, haijabinika ikiwa kidole gumba chake kilikatwa kabla au baada ya kifo chake.