Ndugu zangu,
kwenye gazeti la Mwananchi la leo ukurasa wa tatu kuna habari yenye kichwa cha habari kama ilivyo hapo juu. Bahati mbaya hawajaipost lakini imeandikwa hivi;
Mwanaume ambaye hakufahamika jina lake katika hali isiyo ya kawaida, juzi usiku alitumia fursa ya milipuko ya mabomu kumshawishi msichana aliyekuwa akihaha kutafuta hifadhi akiwa na mdogo wake mgongoni, wafanye vitendo vya ngono......(inaendelea lakini habari kuu ndiyo hiyo)
Huu ni uzandiki kabisa afungwe
Hivi ethics za uandishi wa habari hazimtaki mwandishi akikutana na jambo kama hili ampeleke mtuhumiwa polisi pamoja na kuandhika taarifa husika?
Sasa LD naona hapo umeenda mbali kidogo.
dah! taratibu LD, usije ukavunja skrini kwa hasira.Hapa ndipo ninapowazaga akili za wanaume ziko je??
Kwa sababu hata ikitokea vita utasikia wanawake wamebakwa bila hata huruma!!! Yani mi kuna wakati najiulizaga kwa nini Mungu aliumba wanaume kwa jinsi hiyo!! Daaa mi wanaume nawaogopa aisee!!! Ndio sio wanaume wote wenye roho kama hizi, lakini hebu wote vaeni uhusika halafu muone jinsi ambavyo mpo wa ajabu.
Daaa hapa hakuna cha kusema kaka angu, baba angu au sijui nani angu, so long as is a man!!!!!!! Why this?? Mnaongozwa na roho gani?? Ya Mungu au ya Shetani??
Daaaaaaah. Inauma sana aiseeeee!!!!